Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Kampuni ya Zane Finance imewaomba Watanzania kutembelea katika banda lao lilipo katika jengo la Benjamini Mkapa kwa ajili ya kupata elimu sahihi juu ya mikopo ya ada ya shule na bima inayotolewa na kampuni hiyo.
Akizungumza na Mtanzania Digital kwenye maonyesho ya 45 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam Afisa Masoko wa Zane Finance, Joshua Mizambwa, lengo ni kuona watanzania wanatatua changamoto zao.
Amesema kutokana na changamoto mbalimbali za maisha zinazowakabili Watanzania, kampuni hiyo imekuja na utaratibu wa mikopo kwa ajili ya ada sambamba na ile yawafanyabiashara, wafanyakazi na wajasiriamali lengo likiwa ni kuwezesha kila mmoja kufikia ndoto zake.
Akizungumzia mkopo mpya wa ada ya shule, Mizambwa amesema kuwa Watanzania wengi wamekuwa na shahuku ya kutaka kupata mkopo huo ili kuweza kukamilisha malengo ya kimasomo.
“Tunawakaribisha Watanzania kwenye banda letu kwa ajaili ya kuopata elimu sahihi ya mikopo yetu kwani tuna mikopo ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mteja, kwa sasa tuna mkopo wa ada za shule ambao huu ni mpya na mtu anakopeshwa kuanzia Sh 500,000 hadi 2,000,000 kwa kiwango cha chini.
“Marejesho ya mkopo huu ni kila mwezi dani ya miezi mitatu na tumejikita kwa wafanyakazi sababu wanaweka dhamana ya gari ambapo mzazi anaweza kuchukua mkopo kwa ajili ya mtoto wake wa sekondari.
“Lakini pia kama mwananfunzi mwenyewe ana uwezo wa kuchku mkopo huu tunamkaribisha, kwani kengo ni kupunguza makali ya maisha kwa maana ya ada, hivyo hadi sasa tumefikia asilimia 75 ya mwitikio kwani kama unavojua wanafunzi ni wengi na watu bado hawana fedha,” amesema Mizambwa.
Amesema mbali na mkopo huo wa ada ya shule pia wamekuwa wakitoa mikopo kwa ajili ya biashara lengo likiwa ni kusaidia wafanyabiashara kuweza kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa Tanzania ya Viwanda.
“Pamoja na kwamba kwa sasa ofisi zetu zinapatikana Dar es Salaam na Mwanza lakini mpango wetu ni kuona tukifika mbali zaidi kwa kuongeza matawi lengo likiwa ni kuwasaidia Watanzania.
“Hivyo tuwakaribishe wananchi kutembelea banda letu kwa ajili ya kupata elimu pamoja na mikopo,”amesema Mizambwa.
Kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa huduma za bima kupitia kampuni ya Accept Insurance Broker.