25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania waaswa kutumia chai ya asili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watanzania wameaswa kutumia chai ya asili inayotegenezwa na mimea ya asili ili kuuwezesha mwili kupata kinga sahihi na yenye virutubisho.

Akizungumza katika maonyesho ya 45 ya Kimatafa ya Biashara ya Sabasaba (DTIF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mkurungezi wa Taasisi inayojishughulisha na utoaji wa tiba asili ya Cornewell Tanzania, Elizabeth Lema, amesema unywaji wa chai ya asili iliyotegenezwa kiusahihi inamuwezesha mtumiaji kuimarisha kinga ya mwili.

Amesema kuna aina mbalimbali za chai ya asili ikiwepo Digestive tea, Diabetes tea, Mango leaves tea,Giele Herbal tea, Eucalyptus Herbal tea na Cemon Leaves tea.

Aidha, aliongeza mbali na chai kuna bidhaa nyingine ambazo zinatumia mimea ya asili kutibu magonjwa mbalimbali ambazo zimeboreshwa ili kukuwezesha mtumiaji kupata yenye usahih.

Amewaasa watanzania kutembelea bada lao lililopo katika maonyesho hayo ili waweze kupata maelezo sahihi kutoka kwa wataalamu huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutambua mchango wa tiba asili inayotokana na mimea.

“Naipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuthamini mchango wa tiba za asili na kusema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa usahihi ili kuimarisha afya za watanzania”amesema.

Alisisitiza kuwa kuna magonjwa mengi ambayo yanaweza kutubika kupitia miti dawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles