WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI AMANI WALIYONAYO

0
910
5r5a2270
Watu wakifanya mazoezi ya yoga kuimarisha afya zao

Mkurugenzi wa Brahma Kumaris, Kanda ya Afrika taasisi inayotoa mafunzo ya kiroho na mazoezi ya kuimarisha afya (Yoga), Kumaris Vendanti, amewataka watanzania kuhakikisha wanathamini amani na upendo walionao,  kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Vedanti aliyasema hayo akiwa nchini kwa ziara ya siku chache ambapo pia anategemea kuzunguka bara zima la Afrika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuthamini na kutunza  amani na upendo.

“Ulimwengu wa sasa ni lazima jamii kuwa makini sana hasa linapokuja suala la utandawazi ambapo unakuta mzazi anajikita zaidi kwenye kuandikiana ujumbe kwenye simu, mitandao, au hata kuwaacha watoto wakiangalia runinga badala ya kuwafundisha maadili  bora  kwa manufaa ya maisha yao ya baadae,” alisema.

Akaongeza kuwa kwa kutumia matawi ya taasisi hiyo, watanzania wataweza kupata elimu za kiafya, na maadili mema na hivyo Tanzania ya miaka ijayo kuwa na viongozi wenye maadili mema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here