24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Washindi NMB MastaBata wafikia 400, wajizolea Mil 40

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wateja 400 kati ya 1,080 wanaowania zaidi ya Sh milioni 200 za Kampeni ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ wamepatikana na kujinyakulia pesa taslimu kiasi cha Sh milioni40, baada ya droo ya Wiki ya Nne kufanyika na kuzalisha washindi 100.

‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ ni kampeni inayolenga kuhamasisha  matumizi na malipo kwa njia ya kadi za MasterCard, Masterpass QR, Vituo vya Mauzo (PoS) na mtandaoni, njia ambayo ni salama na nafuu zaidi kulinganisha na pesa taslimu.

Katika kampeni hiyo, kila wiki washindi 100 hujishindia Sh 100,000 kila mmoja, huku washindi 25 wa mwisho wa mwezi wakizawadiwa Sh milioni 1 kila mmoja, wakati ‘Grande Finale’ itakuwa na wateja 30 watakaotwaa Sh milioni 3 kila mmoja.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa droo ya nne jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 28, 2021, Meneja wa Kitengo cha Kadi  NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema idadi ya wateja wanaoshinda pesa, inaongezeka kadri droo zinavyochezeshwa, ingawa bado idadi ya wateja waliobakia ni wengi.

“Leo tunafikisha idadi ya wateja 400 walionufaika kwa zawadi za kampeni hii inayofanyika kwa msimu wa tatu sasa. Hii maana yake ni kuwa tumebakisha zaidi ya washindi 680, tutakaowapata kupitia droo sita za wiki, mbili za mwezi, pamoja na fainali kuu itakayofanyika mwishoni mwa kampeni.

“Kila wiki tunawazawadia washindi 100, ambao kila mmoja anapata Sh 100,000, kila mwisho wa mwezi washindi 25 watakaopata Sh milioni 1 kila mmoja na fainali washindi 30 wataojinyakulia Sh milioni 3 kila mmoja. Kila mteja anayetumia kadi na PoS ana nafasi sawa ya kushinda, wito wetu kwao ni kuwataka waendelee kufanya manunuzi na malipo kwa kadi,” amesema Mwamwitwa.

Droo hiyo ya nne ya NMB MastaBata ilifanyika chini ya uangalizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), iliyowakilishwa na Rasuli Masudi, ambaye alisisitiza kuwa uwepo wa bodi yake katika droo hizo, unaakisi matumizi ya sheria, kanuni na taratibu za michezo hiyo nchini.

“Niko hapa kwa niaba ya Bodi, ambayo wajibu wake ni kuhakikisha sheria na taratibu zinazosimamia michezo hii zinafuatwa. Wateja wa NMB wawe na uhakika kuwa kampeni hii inafanyika kwa kufuata kanuni za GBT,” amesema Masudi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles