25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Matukio ya ubakaji kwa wanafunzi yaongezeka Ludewa

Na Elizabeth Kilindi,Njombe

Zaidi ya kesi 57 za ubakaji kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zimeripotiwa wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe katika kipindi cha mwaka 2021.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere, ambapo amesema kuwa matukio hayo yamekua yakijitokeza zaidi kwa wanafunzi wa darasa la sita hadi kidato cha nne.

“Jambo hili linajirudia mara kwa mara kwa sababu pia linachangiwa na na jamii,mara nyingi kesi za ubakaji zimekua zikishindwa kupata ushahidi kwa sababu mara tu tukio linapotokea linaporipotiwa tunahitaji jamii itoe ushirikiano ili tupate ushahidi.

’’Lakini jamii mara nyingi wanaamua kukutana wenyewe, wanaamua kukubaliana mbakaji anatoa fedha anamuonga mzazi wa mtoto aliyeathirika alafu mwisho wa siku wanasema tunamalizana huku. Ukimtafuta anakwambia mimi nitaonekanaje kwenye jamii nikiendelea kufuatilia kesi hiyo, mwisho wa siku yule mtoto anatoroshwa,’’amesema Tsere.

Mkuu wa wilaya hiyo amesema kwa kufanya hivyo hatutaweza kupambana na kuzuia tabia ya ubakaji kwa watoto na kwamba kama wabakaji wataendelea kufichwa jambo ambalo itakua ni hatari.

“Ili kukomesha tabia hii, tabia hii haitakoma kama tutaendelea kuwaficha kama tutaendelea kusema wametoroka kama tutaendelea kusema hii mimba haijulikani mtu wake hii tabia haitakoma na tutaendelea kupoteza watoto wetu na hawatasoma, watoto wengi watakatishwa shule,ndoto za watoto zitakua zimekufa, viongozi wakubwa tunawamaliza kwa kuwabaka,tunawarudisha nyumbani wanakua ni watoto wa kazi,” amesema Mkuu wa wilaya ya Ludewa.

Awali, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa, Deogratius Masawe,alikiri kupoke kesi nyingi za ubakaji ambazo zinasababisha mimba na hivyo kuwafanya wanafunzi kusundwa kuendelea na masomo.

“Naomba ushirikiano kutoka kwa madiwani najua mnaweza kupeleka elimu kwa watu mbalimbali ili kuhakikisha changamoto hiyo inamalizika na watoto waweze kutimiza ndoto zao,’’ amesema Masawe.

Maria haule ambaye ni mzazi mkazi wa Ludewa mjini alisema kukosekana kwa maadili kwa vijana ndio sababu ya kushamiri kwa vitendo vya ubakaji.

“Binti akiwa ametulia nyumbani anajiheshimu anashirikiana na mzazi hawezi kukutwa na haya majanga,wazazi wajitahidi kukaa na mabinti zao kuwaelekeza maadili mema mtoto wa kike anatakiwa kulindwa na mazazi,” amesema Maria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles