26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii watakiwa kununua stempu za kodi

 Moses Mwanyilu
Moses Mwanyilu

NA FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM

CHAMA cha wasambazaji filamu nchini kimesema kila msambazaji au msanii anapaswa kununua stempu za kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TCRA), kabla ya kuziiingiza sokoni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Moses Mwanyilu, alisema baada ya kupitia hatua mbalimbali kama vile BASATA kwa kazi za muziki, COSOTA na bodi ya filamu kwa ajili ya ukaguzi, zibandikwe stempu kabla ya kuingizwa sokoni.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara na wasambazaji wa muziki kutoka nje ya nchi wamekuwa wakiingiza na kuuza bidhaa hizo bila kufuata utaratibu, ikiwemo kutolipia kodi na kuuza kwa bei ya chini ukilinganisha na filamu za hapa nchini na kusababisha soko la filamu za ndani kushuka.

“Filamu za nje zimekuwa hazina maadili ya Tanzania na filamu za ndani wanadurufu na kuziingiza sokoni bila wasanii kunufaika na kazi zao.

“Tunapenda kutoa shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kufanya operesheni ya kukamata kazi ambazo zinauzwa kinyume cha sheria katika eneo la Kariakoo,” alisema.
Hata hivyo, wameiomba Serikali operesheni hiyo iwe endelevu katika maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles