22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Zidane apishana kauli na rais wa timu

Zinedine Zidane
Zinedine Zidane

MADRID, HISPANIA

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amepishana kauli na rais wa timu hiyo, Florentino Perez, baada ya kocha huyo kumuacha nyota wa timu hiyo, Martin Odegaard.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17, Zidane, hakumuita katika kikosi chake ambacho kimeelekea nchini Canada kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi.

Inadaiwa kwamba Zidane na mchezaji huyo wamekuwa hawana maelewano mazuri tangu Januari mwaka huu, hivyo japokuwa ana uwezo mzuri, lakini aliachwa katika kikosi hicho.

Perez anaamini kuwepo kwa mchezaji huyo katika kikosi hicho ataifanya klabu hiyo kuzidi kuwa na mashabiki katika ziara hiyo, pia anaweza kupata klabu ya kuitumikia katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Zidane anamtaka mchezaji huyo kujiunga na klabu nyingine kwa mkopo na ndiyo maana hakutaka kumuita katika kikosi chake.

Inadaiwa kwamba watoto wawili wa Zidane, Luca na Enzo, wapo katika ziara hiyo ya Real Madrid nchini Canada, wakati huo wachezaji hao wanatumikia timu B, ambayo inajulikana kwa jina la Castilla.

Hata hivyo, baada ya Zidane kupishana kauli na rais wake, baada ya muda waliyamaliza, hivyo mchezaji huyo amejiunga na klabu hiyo katika ziara hiyo na sasa wapo jijini Montreal.

Odegaard alijiunga na Real Madrid, Januari 2015, lakini ilipofika Aprili mwaka huo alishushwa hadi timu B, ila baada ya muda aliitwa tena kwenye kikosi hicho na alipata nafasi kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Gatafe, ambapo aliingia akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo, huku timu hiyo ikishinda mabao 7-3.

Wachezaji ambao Zidane amewaita katika kikosi chake ni pamoja na walinda milango ambao ni Navas, Casilla, Ruben Yanez, Craninx, Luca Zidane, wakati katika safu ya ulinzi ni Varane, Danilo, Carvajal, Marcelo, Nacho, Lienhart, Tejero, Achraf, huku kiungo akiwa Casemiro, Isco, Kovacic, Llorente, Asensio, Odegaard, Enzo, Febas na washambuliaji ni Benzema, Jese, Mayoral, Mariano.

Ratiba yao ni kucheza dhidi ya PSG Julai 28, huku Julai 30 wakicheza dhidi ya Chelsea, Agosti 3 wakicheza dhidi ya Bayern Munich.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles