WASANII wa fani mbalimbali, wachezaji wa soka Ligi Kuu Tanzania Bara na wadau wa afya leo wanaungana katika bonanza la kuadhimisha mwezi wa kuongeza uelewa juu ya ugonjwa wa upungufu wa damu (sickle cell).
Wasanii watakaokuwepo katika bonanza hilo ni Wema Sepetu, Banana Zorro, Barnaba, Mwana Fa, Vyone Cherry (Monalisa).
Wengine ni mshindi wa tuzo mbili za ZIFF, Honeymoon Mohammed, Miss Tanzania mwaka 1998, Basila Mwanukuzi na kwa upande wa soka watakuwepo baadhi ya wachezaji wa Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Deogratias Soka, alisema mwezi ujao ni mwezi unaotumika kwa maadhimisho ya ugonjwa huo nchini.
“Kesho (leo) tunafanya bonanza ambalo nia yake ni kuadhimisha mwezi wa kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo huku lengo kuu likiwa ni kuhamasisha watu kupima na jamii ifahamu kuhusu ugonjwa huu.
Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuanzisha kampeni ya upimaji wa watoto wa ugonjwa huo na katika bonanza hilo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.