28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wapinzani waungana Uganda

KAMPALA, Uganda 

VIONGOZI  wa vyama vya upinzani nchini Uganda, Kanali Dk. Kizza Besigye na Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, wameunda muungano wa upinzani.

Robert Kyagulanyi wa Chama cha People Power kwa pamoja na Dk. Kizza Besigye ambaye chama chake FDC kinaongozwa na Amulati, Meya wa Kampala, Erias Lukwago wa Chama cha DP, Rais wa Chama cha CP, Keny Lukyamuzi, Rais wa Chama cha JEEMA, Asumani Bsalirwa na wengine wengi wamezindua rasmi muungano mpya wa upinzani  ambao utasisimisha mgombea mmoja katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mwakani dhidi ya Rais Yoweri Museveni.

Akizindua rasmi muungano huo katika Wilaya ya Wakiso, Kyagulanyi alisema muungano huo  ambao unajulikana jina la ‘United forces of change’ na kwamba hadi hapo walipofika wameepiga hatua kubwa.

“Nashukuru viongozi wetu walioona njia, wakafuata njia hiyo na kutuonyesha njia,” Kyagulanyi alisema 

”Lazima tushirikiane kwa manufaa ya nchi yetu.” Kyagulanyi ameongeza hayo huku akisisitiza kuwa njia walioshika ndio sahihi.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mbunge, ameweka wazi  wao (walioungana) sio maadui na kadiri wanavyoendelea kupigana vita wenyewe kwa wenyewe ndivyo wanavyoendelea kuchelewesha mabadiliko ambayo raia wamekuwa wakisubiri kwa hamu.

Alisema ili kufikia wanacholenga kunaweza kufanikiwa tu kwa kama watashirikiana na watu.

”Natoa wito kwa raia wote wa Uganda, msilale badala yake mpaze sauti zetu,” alisema.

Katika hotuba yake, amemnukuu Malcolm X ambaye alikuwa mwanaharakati wa haki za kiraia za Waafrika-Waamerika ”Mikakati inaweza kutofautiana, hatua za kuchukua na mbinu zinaweza kutofautiana lakini lengo likawa moja.”

Viongozi wa vyama viwili vikuu vya upinzani, Kanali Besigye na  Kyagulanyi, wamekuwa wakikutana mara kadhaa kuandaa mikakati ya kuunda muungano huo wa “United force of change”.

Wabunge wengine pamoja na wafuasi wao ni miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi huo.

Na wale waliokuwepo walifuata kanuni ya kutokaribiana ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona.

Lakini mkutano huo, umesambaratishwa na polisi dakika za mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles