24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wapinzani wamwita Prof. Tibaijuka mwizi  

TibaijukaNa Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amekumbana na wakati mgumu bungeni baada ya kuzomewa na kuitwa mwizi na wabunge wa upinzani.

Profesa Tibaijuka alikumbana na hali hiyo, wakati akichangia mjadala wa hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa na waziri wake, Dk. Harrison Mwakyembe bungeni mjini hapa jana.

Kutokana na zomea zomea hiyo, kila wakati Profesa Tibaijuka alilazimika kumwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai amlinde.

Akichagia mjadala huo, alisema wabunge wanaomwita mwizi, kwake wataisoma namba kwa kuwa hatishwi na vitu vya ovyo ovyo.

Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema amepitia mapito mengi.

“Kwanza wale wanaosema mimi nimeiba, hapa kwangu wataisoma namba… mimi siyo mtu wa kutishwa na vitu vya ovyo ovyo. Kama kuna mtu anafikiria naweza kutishika kwa hoja za ovyo aisome namba,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, kila wakati Profesa Tibaijuka alilazimika kumwomba Spika wa Bunge, Job Ndugai amlinde.

Akijibu hoja za Kambi Rasimu ya Upinzani Bungeni, iliyowasilishwa na msemaji wake, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Tibaijuka alisema madai kuwa Tanganyika inainyonya Zanzibar hayana msingi wowote.

Alisema ni hatari kwa mtu kuupotosha umma kwa kusema Tanganyika inainyonya Zanzibar kwa kuwa kiuchumi suala hilo haliwezekani.

“Upinzani ukifilisika ukabaki sasa kukemea kwa sababu lazima useme kitu, Bunge linageuka kijiwe, hapa hatuleti hoja za vijiweni. Kwa mfano kusema Tanganyika inainyonya Zanzibar, inainyonya katika lipi hili?

“Ni jambo la kujiuliza hapa, kazi yangu ya kwanza ilikuwa kwenye Shirika la Sera la Duniani  nikisimamia uchumi, mbona sikusikia jambo kama hili,” alisema.

Alishangazwa na hotuba ya upinzani na kusema ni ngumu kwa Zanzibar kusimama kiuchumi na hatimaye siku moja iwe kama Singapore, kwani haina bandari ya uhakika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles