27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wapinzani waiburuza serikali mahakamani


Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Vyama vinane vya kisiasa nchini vimefungua shauri la kupinga Sheria ya Vyama vya Siasa katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) lililopewa namba 03/2019.

Sheria hiyo namba 1 ya mwaka 2019 ilisainiwa na Rais Dk John Magufuli Februari 13, mwaka huu baada ya muswada wa sheria hiyo kupitishwa na Bunge mwaka jana.

Akizungumza katika mkutano wa vyama hivyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 15, kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia a Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema waliamua kwenda katika mahakama hiyo kwani kuna ukomo wa kupeleka mashauri na shauri lao limepokelewa na wamempa siku 45 Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujibu maombi yao.

“Kupitia maombi tuliyowasilisha mahakamani hapo katika shauri hilo tumeiomba mahakama itamke kwamba vifungu tunavyolalamikia havina hadhi ya kisheria, tumelazimika kuitafuta haki kutokana na kuwa sheria hiyo ni mbaya na ambayo inafanya shughuli za kisiasa nchini kuwa jinai.

Msingi wa madai yetu katika shauri hilo ni kwamba sheria ni mbovu na inakiuka misingi ya mkataba y uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hususani katika ibara ya 6, 7 na 8B ya mbali na hilo pia inakiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na misingi ya utawala bora na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo nchi imetia saini, “ amesema.

Katika hatua nyingine Mbowe amesema kanuni mpya za chaguzi za Serikali za Mitaa zinawanyima haki wapinzani kwani hawaruhusiwi kwenda kufanya kampeni na mikutano ya kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini.

Tunaingiaje katika uchaguzi bila kujijenga miaka minne sasa hatujajijenga kwa mikutano, hatuwezi kufanya uchaguzi kwa kampeni za siku Saba tena karibia na uchaguzi,” amesema.

Aidha vyama hivyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Chama cha wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, Chama cha National League for Democracy (NLD) na Chama cha Kijamii (CCK).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles