23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Upinzani wamtaka Spika ajiuzulu


Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Vyama vinane vya kisiasa nchini vimemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai ajiuzulu kutokana na kauli yake ya kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) Profesa Musa Assad akamuombe msamaha Rais Dk. John Magufuli au ajiuzulu kwani kufanya hivyo ni kushindwa kazi.

Vyama hivyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, Chama cha National League for Democracy (NLD) na Chama cha Kijamii (CCK).

Akizungumza katika mkutano wa vyama hivyo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 15, kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP), Fahmi Dovutwa amesema kauli hiyo ya Spika ni kutaka kuichanganya ofisi ya Rais na Bunge.

“Desturi tuliyoachiwa na Hayati Baba wa taida Mwl. Julius Nyerere ni kuwa viongozi wakubali kukosolewa na wasijisie vibaya wanapokosolewa, kauli ya Spika ya kumtaka CAG ajishushe kwa Rais ama kujiuzulu sio nzuri, taaifa haliwezi kwenda namna hii.

“Leo ameanza na CAG, kesho atasema IGP na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi wajiuzulu, hii inaonesha Splika ameshindwa kazi hivyo ni bora ajiuzulu yeye,” amesema Dovutwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amesema kauli ya Spika ni yake binafsi na si msimamo wa Bunge kwasababu kama wabunge hawakukaa bungeni na kujadili wamwambie CAG ajiuzulu.

“Spika ameligeuza Bunge ni chombo chake binafsi, wabunge wanafukuzwa bungeni hovyo, mbunge anapofanya kitu kisichokupendeza wewe usisahau kuwa yule ni muwakilishi wa wananchi, pamoja na udhaifu wake Bunge halijamtuma akamwambie CAG ajiuzulu huo ni mtazamo wake binafsi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles