27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waondokana na adha kutembea kilomita 20 kufuata shule

Na Mwandishi Wetu -Kilwa

WATOTO wanaoishi katika Kitongoji cha Mbeta, Kata ya Kikole, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wameondokana na adha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 20 baada ya Kampuni ya uchimbaji gesi ya Pan African Energy Tanzania kuwajengea shule.

Shule hiyo iliyojengwa katika Kitongoji cha Mbeta, Kijiji cha Migeregere itatumika kwa wanafunzi wa madarasa ya awali hadi la pili kisha watahamishiwa katika shule mama ya Migeregere.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja Uwajibikiji kwa jamii wa kampuni hiyo, Andrew Kashangaki, alisema wamejenga madarasa sita, vyoo vitatu, ofisi mbili za walimu na madawati 138 vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 300.

Alisema waliguswa na hali iliyokuwepo kijijini hapo ambapo wanafunzi walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita 10 ili kufika ilipo shule ya sasa ya Migeregere hali iliyosababisha mahudhurio kuwa mabaya pamoja na usalama mdogo wa wanafunzi wakati wa kwenda na kurudi nyumbani.

Diwani wa Kata ya Kikole, Musa Kinjokwile, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwajengea shule kwani watoto wengi walikuwa hawaendi shule kutokana na umbali uliopo.

“Ndugu zangu mimi sina cha kuwalipa, kijiji hiki hakijawahi kuwa na majengo ya aina hii na wananchi walishakata tamaa kuishi katika kijiji hiki kutokana na changamoto za huduma za kijamii ikiwemo shule,” alisema Kinjokwile.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Renatus Mchau, aliwataka wananchi kuzingatia elimu kama njia pekee na ya kisayansi inayoweza kuwasaidia kujikwamua katika umasikini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles