26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wanne mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Na Hadija Omary, Lindi

Jeshi la Polisi mkoani Lindi linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukutwa na kilo 261 za meno ya Tembo yenye thamani ya Sh milioni 69.5, Mkonga mmoja wa tembo, vipande 87 vya nyama ya tembo, bunduki moja aina ya Rifle 375 maganda ya risasi saba na vichwa vya risasi sita, risasi moja inayodhaniwa kutengenezwa kienyeji na mitego ya waya “Roda” tisa.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amesema kuwa tukio hilo limetokea Machi 17, mwaka huu katika Kijiji cha kiangala kata ya kibutuka wilayani Liwale mkoani Lindi.

Kamanda Kitinkwi amesema kushikriwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na msako ulioendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na  mamlaka ya Wanyama pori Tanzania (TAWA) katika muendelezo wa kudhibiti vitendo vya ujangili ambapo lilianzisha msako mkali katika Wilaya hiyo ya Liwale.

Kitinkwi ameeleza kuwa baada ya Mtuhumiwa wa kwanza alietambulika kwa jina la Mohamedi kuhojiwa kwa kina alieleza kuwa tembo hao wawili waliwawinda katika mapori ya wazi ya Nyera kipelele (TFS) na (Hangai) Chini ya kijiji yaliyopo kata ya kiangara wilayani Liwale mkoani Lindi.

Hata hivyo, Kitinkwi alifafanua kuwa watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi mpaka pale upelelezi utakapo kamilika kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wake kamanda wa uhifadhi wa wanyama Ppri kanda ya Kusini Mashariki, Abraham Jullu amewataka wananchi kutoa taarifa kwa taasisi zinazohusika pindi wanapoona Wanyama wameingia kwenye maeneo ya makaazi ya watu.

Amesema baada ya mamlaka hiyo kuimarisha ulinzi latika maeneo ya hifadhi kwa lengo la  kudhibiti vitendo vya ujangili, hivi sasa majangili hawaingii tena katika maeneo hayo ya hifadhi.

“Kwa uzoefu wangu mara nyingi wanayama wanaouliwa ama kuwindwa na majangili ni wale waliotoka nje ya misiti ama maeneo ya hifadhi za mamlaka hizo na kwenda nje  ya maeneo ya hifadhi, hivyo nitoe wito kwa wananchi kutoa taarifa jwa mamlaka zinazohusika pindi tu wanapoona wanyama katika maeneo yao ili tuweze kuudhibiti majangili kwa manufaa ya nchi,” amesema Jullu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles