26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake walalamikakwa mke wa Lowassa

Pg 22 sept 18Na Mwandishi Wetu, Meatu

WANAWAKE wilayani Meatu mkoani Simiyu wamelalamikia kitendo cha kuuziwa kadi za kliniki Sh 3,000, wanapokwenda kupata huduma ya kupimwa.

Hali hiyo, imesababisha wajawazito wengi washindwe kuhudhuria kniliki kwa sababu ya kukosa fedha. Wakizungumza kwa masikitiko mbele ya mke wa mgombea urais kwa wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa,mama Regina Lowassa, akina mama hao walisema wanashindwa kuanza kliniki kutokana na gharama kubwa.

Walisema baadhi ya wauguzi katika hospitali za serikali mkoani Simiyu, wamekuwa wakidai fdeha ili wawapime . Mmoja wa akina mama hao, Fatuma Selmani alisema kuna baadhi ya akina mama amepoteza maisha kutokana na kutokuhudhuria kliniki, kwa sababu wengi wao wanajifungulia majumbani Walisema kero nyingen, walisema wamekuwa wakizuiwa na mabwana shamba wasilime kilimo cha mseto kwa kuchanganya mahindi na pamba.

Alisema kutokana na ukame, wanalazimika kulima kilimo cha kuchanganya mazao ili waweze kujikinga na njaa Naye Teresia Edward mkazi wa kijiji cha Miringi,alisema wamechoshwa na uonevu huo.

Kwa upande wake, mama Regina alisema kuna haja ya Serikali kusikia kilio cha akina mama hao, kwani kwa wajawazito ni muhimu ndiyo maana kadi hutolewa bure.

Kuhusu elimu, alisema kila mtoto atasoma bure kwa sababu Ukawa wamedhamiria kuondoa tatizo la watoto kukosa shule. “Wanawake wenzangu naomba mwaka huu msiniangushe Oktoba 25, mpeni kura za ndiyo Lowassa ili apate ridhaa ya kuongoza,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles