27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake Cameroon wanavyokumbana na changamoto lukuki kulima mpunga

KilimoWANAWAKE kundi ambalo linaelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika shughuli za kiuchumi ikiwamo kilimo katika mataifa mengi ya Afrika ambapo suala hili limekuwa likinyimwa uzito ili kuboresha kilimo chao.

Miongoni mwa mataifa hayo ni Cameroon, ambako wakulima wanawake licha ya kuwa tegemeo la uzalishaji wa zao la mpunga, wanatumia vifaa duni vya kufanyia kazi.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa wanawake katika taifa na hivyo kuwarudisha nyuma kimaendeleo, kwa wanaume hali ni tofauti kwa vile wao ni rahisi kupata kile wakitakacho katika kuboresha kilimo chao.

Hiyo ni changamoto ya mfumo dume ambao umekuwa ni chanzo cha dhuluma na manyanyaso dhidi ya wanawake barani Afrika.

Lakini kwa uhakika kabisa, wanawake wakiwezeshwa katika afya, elimu na uchumi, umaskini barani Afrika unaweza kupewa kisogo.

Ingawa mwanamke ni nguzo kubwa na muhimu katika maisha na maendeleo ya mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.

Pamoja na ushuhuda uliotolewa na mashirika mbalimbali ya kimataifa huku ikijulikana ukuaji wa maendeleo ya Bara la Afrika hauwezi kutokea bila kuwahusisha wanawake kama wadau wakuu katika mchakato huo, wengi bado wanapuuzwa.

Kwanini mpunga? Ni zao linalozalishwa kwa wingi barani Afrika na duniani kwa ujumla wake kwa vile huliwa na watu wa jamii mbali mbali duniani.

Ni zao la pili la nafaka linalozalishwa kwa wingi katika sayari hii baada  ya  mahindi.

Lakini kwa vile mahindi huzalishwa kwa ajili  ya  matumizi mengine zaidi ya chakula hivyo, kuna uwezekano kuwa mchele unaongoza kwa kutumiwa kama lishe duniani.

Hali kadhalika mpunga  unaweza  kutumika  kama  zao la  chakula  na  biashara  na  ni  muhimu  katika  kujenga  afya  ya  mwili.

Aidha mpunga licha ya mara nyingi kuwa na bei nzuri kulinganisha na mahindi hutoa mavuno mengi kuliko nafaka hiyo ya mahindi.

Tukirudi katika changamoto zinazowakabili wakulima wanawake nchini Cameroon;

Tuchukulie simulizi ya mwanamke huyu mkulima nchini Cameroon; kwa zaidi ya miaka 20, sasa, Anastazia Ngwaun kutoka katika kijiji cha Bamunkumbit nchini humo, amekuwa akilima zao hilo huku akikabiliwa na changamoto mbali mbali.

Changamoto hizo ni pamoja na kulima kwa kutumia teknolojia iliyopitwa na wakati yaani; jembe la mkono.

Mwenyewe anaamini angekuwa mwanaume ingekuwa rahisi kwake kuifikia teknolojia ambayo ingemrahisishia kufanya kazi hiyo kwa haraka, ufanisi na kwa eneo kubwa.

Kwa sababu hiyo anasema kilimo cha mpunga ni kazi ngumu mno, hususan kwa wanawake licha ya kuwa na faida za kijamii na kiuchumi iwapo kutakuwa na mipango bora.

Mkulima huyo anasema anajihusisha na upandaji na hatua nyingine zote za kuzalisha mpunga kwa kutumia vifaa duni au kuvikosa kabisa.

Anasema tofauti na wanawake kama yeye, wanaume wanaojihusisha na ukulima wa zao hilo katika kijiji hicho, inawawia rahisi kwao kupewa mikopo au kupata matrekta ya kurahisisha kazi yao.

Mkulima huyo ameliambia Shirika la Habari la IPS kuwa wanawake wana matatizo mengi, kwani hawana mamlaka ya kumiliki ardhi na kujikuta mara nyingi wakilima kwenye mashamba yanayomilikiwa na wanaume.

Anasema pia wanaelekezwa kulima maeneo yanayolimwa kwa kutumia matrekta na kwa sababu hiyo ni wazi kuwa wanaotumia matrekta watamaliza kwanza ndipo wanawake wafuate nyuma.

Biashara ya mpunga CameroonAnasema kilimo cha mpunga kingekuwa rahisi kwake ikiwa angekuwa na teknolojia ya kumrahisishia kufanya kazi kama vile mashine ya kupukuchua mpunga, vifaa vya kupalilia magugu na vifaa vingine muhimu vinavyotumika katika kilimo hicho.

Lakini bahati mbaya sana kama ilivyo kwa wanawake wengi Afrika, hana uwezo wa kuvipata kirahisi.

Kutokana na matokeo ya utafiti uliofanywa na kituo cha utafiti wa zao la mpunga, kanda ya Afrika unaonyesha kuwa ikilinganishwa na wanawake, wanaume katika sekta ya kilimo wana nafasi kubwa ya kupata rasilimiali kama vile umiliki wa ardhi, kupata mitaji, elimu na vifaa vya kisasa vya kilimo.

Hilo pia linachangiwa na tamaduni zilizopo na uwezo kiuchumi.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya jinsia katika kituo hicho, Afiavi Aghbor-Noameshie, hakuna mfumo mzuri wa kijinsia katika sekta ya kilimo cha mpunga barani Afrika.

Hiyo ni pamoja na kwamba wanawake wanashiriki kikamlilifu katika shughuli zote za kilimo hicho kuanzia kwenye kupanda hadi kutafuta masoko, lakini hawapewi kipaumbele katika suala la teknolojia.

Kwa sasa, Afrika inaongoza kuagiza mchele kutoka nje kutokana na kutumia zaidi ya kile inachozalisha.

Kwa mfano mwaka jana bara hili lilitumia jumla ya dola bilioni tano za Marekani kuagiza tani 12 za mchele kutoka nje licha ya kwamba lina uwezo wa kujilisha lenyewe iwapo mikakati ikiwamo ya kuwezesha wanawake itawekwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles