25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE BURUNDI WAMWANGUKIA MKAPA

Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini Mkapa

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA

BAADHI ya wanawake nchini Burundi, wamemwangukia mwezeshaji wa mazungumzo ya kutafuta amani nchini humo, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini Mkapa, wamkitaka aruhusu ushiriki wao katika mazungumzo hayo.

Kauli hiyo waliitoa mjini hapa jana wakati wa mazungumzo ya kutafuta amani ya Burundi yanayodaiwa kushirikisha idadi kubwa ya wanaume katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wenzake mbele ya vyombo vya habari kutoka ndani na nje ya nchi, Vestine Mbundagu, alisema mazungumzo hayo yamewatenga wanawake wa Burundi ingawa nao ni wadau muhimu wa kutafuta amani.

Alisema mikutano hiyo imekuwa ikihusisha wanasiasa, viongozi wa mashirika, vyama vya siasa na wadau wengine bila kuangalia nafasi muhimu ya wanawake nchini humo.

“Katika mazungumzo yanayoendelea, ukifanya uchunguzi wa kina kabisa utabaini kuna wanawake wawili tu kati ya wanaume 33 na ukifuatilia historia, utagundua wanawake ndio waathirika wakubwa wa vita na machafuko yanapotokea.

“Kama ukweli ndiyo huo, kwanini kwenye meza ya majadiliano ya kutafuta amani wasitushirikishe wanawake?

“Kwa hiyo, tunataka na sisi wanawake tushiriki mikutano yote ya kutafuta amani ya Burundi kwa sababu sisi ni wadau muhimu,” alisema Mbandugu.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Siasa cha Upinzani nchini Burundi (ADAR), Mathias Basabosae, akizungumza nje ya majadiliano hayo aliwataka washiriki katika majadiliano hayo kuwa makini, huku wakitanguliza masilahi ya wananchi wa Burundi.

“Tunahitaji kila mtu aweke mbele masilahi ya wananchi wa Burundi ili wapate amani na waweze kuishi kwa amani nchini kwao,” alisema Basabose.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles