24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume watakiwa kutobaki nyuma Saratani mlango wa kizazi

Na Faraja Masinde, Bukoba

WANAUME mkoani Kagera wametakiwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuwahimiza wenzi wao waweze kufanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.

Wito huo umetolewa juzi mkoani Kagera na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Moses Machali wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhamasishaji wanawake wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi kupima saratani ya mlango wa kizazi.

Machali amesema ni muhimu kwa wanaume kuwahimiza wenza wao kwenda kutazama afya zao kwa kufanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.

“Sisi wanaume pamoja na wake zetu tunao wajibu wa kuihamasisha jamii kuitikia kwenda kufanya uchunguzi ili tuweze kulitokomeza tatizo hili. Nawaasa wanaume wawashauri wake zao kwenda kupima ugonjwa huu ambaonunagharimu maisha yao bila ulazima,.

“Kama kuna wanaume ambao wanaozuia wake zao kwenda kupima waache tabia hiyo mara moja badala yake wawasukume waende wakapime tena wawe wakali pale ambapo wake zao hawataki kuelewa na kwenda kufanya uchunguzi kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewasaidia akina mama na sisi tutaishi maisha yenye furaha sababu hapatakuwa na mgonjwa ndani yake.

“Hivyo ni wajibu wa kila mwanaume kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa familia inakuwa na uhakika wa afya, hivyo ni wajibu wa kila mwanaume kuhimiza mwenza wake katika hili ili kujihakikishia usalama wa afya,” amesema Machali.

Aidha, Machali ameongeza kuwa wanaume kazi yao kubwa ni kuhakikisha kuwa wanawake wanapima na kwamba iwapo wao wataweka mkazo basi itakuwa rahisi.

“Bahati nzuri tuna vituo tumeambiwa ambavyo ni bure, wanaume kazi yetu kubwa ni kuhakikisha wake zetu wanapima kwani mara nyingi wanawake wakipeleka wazo nyumbani huwa halina uzito tofauti na baba ambapoa akipeleka linakuwa na uzito na linafanyiwa kazi kwa haraka,” amesema.

Akiweka msisitizo kwenye hilo la kuhimiza wananume kuwakumbusha wenzi wao, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Safina Yuma amesema amesema kuwa ni busara kwa wnaume kuhimiza wenza wao kufanya uchunguzi.

“Saratani kuna wanaume ambao wanaweza kuwaelimisha wenza wao na wakaenda kupima, hivyo ni jukumu la mwanaume pia katika kuhakikisha kuwa afya ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi inapewa kipaumbele katika familia hatua inatakayo saidia kufikia lengo la kuutokomeza ugonjwa huu,” amesema Dk. Yuma.

Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango.

Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango amesema kuwa uhusika wa wanaume ni muhimu katika kufanikisha lengo hilo.

“Uhusika wa wanaume ni kitu muhimu sana, hivyo pamoja na kuwahimiza wanawake kufika kwenye vituo vya uchunguzi, baodi ni muhimu pia kwa wanaume kushirikiana bega kwa began a wenza wao wanawake ili kusaidia kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huu ifikapo 2030,” amesema Issango.

Mradi huo unatekelezwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali linalosaidia Wanawake waishio na Virusi Vya Ukimwi Mkoa wa Kagera (AMWAVU) kwa kushirikiana na TACAIDS na kufadhiriwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uwezeshaji wa Wanawake, (UN-WOMEN).

Lengo la mradi huo ni kufikia wanawake 600 hususan wanaishi na VVU hadi kufikia Desemba, mwaka huu, huku dhamira ya serikali ikiwa  ni kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles