30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume hatarini kupata saratani ya matiti

NA VERONICA ROMWALD


-DAR ES SALAAM

SARATANI ya matiti huwakabili jinsi zote, wanawake ikiwa ni kiwango cha asilimia 99 na asilimia moja pekee ikiwa ni  wanaume, imeelezwa.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam juzi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Maguha Steven alipozungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu.

Alisema   kila mwaka huwa na uhamasishaji wa umma kuhusu saratani.

“Tupo  Oktoba ambao kila mwaka umetengwa maalumu kwa ajili ya kuhamasisha jamii hasa wanawake kuchunguzwa na kuelimishwa kuhusu saratani ya matiti.

“Ingawa ni saratani inayowapata jinsi zote mbili (kike na kiume) lakini takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonyesha kwa asilimia 99 huwapata wanawake huku wanaume ikiwa ni asilimia moja tu,” alisema.

Dk. Maguha alisema tathmini ya ORCI inaonyesha hivi sasa jamii imekuwa na mwamko mkubwa wa kuchunguzwa afya tofauti na ilivyokuwa awali.

“Kwa kweli tunavishukuru mno vyombo vya habari kwa kushirikiana nasi kuelimisha jamii, hapa ORCI tunapokea wanawake wapatao 80 kila siku ambao huja kuchunguzwa saratani ya matiti.

“Wanaume nao hawapo nyuma huja kule kitengo cha uchunguzi kuchunguzwa iwapo wanakabiliwa na saratani ya tezi dume au la.

“Hii inamaanisha kwamba elimu imewafikia na wamehamasika kwa sababu saratani zote zinatibika hasa zinapogundulika mapema,”alisema.

Alisema katika kuadhimisha mwezi wa uhamasishaji uchunguzi saratani ya matiti ORCI inawaalika wananchi kujitokeza na huduma hiyo inatolewa bila malipo.

 

V

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles