25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaojimilikisha mali za urithi Ilala waanza kusakwa

Na Tunu Nassor, Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Ilala, imeanza kuwasaka na kuwashughulikia watu wote waliojimilikisha viwanja na nyumba za urithi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam kinyume na utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 15, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watu kwa kushirikiana na ndugu wa mbali wa familia kudhulumu viwanja na nyumba zinazoachwa na marehemu.

“Natoa onyo kwa wale wote ambao wamekwa wakijimilikisha nyumba na viwanja hasa katika eneo la Kariakoo, tumeanza ufuatiliaji kuwabaini hasa wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu,” amesema Myava.

Amesema taasisi hiyo inatoa onyo pia kwa waajiri ambao wamekuwa hawapeleki michango ya waajiriwa katika mifuko ya jamii na kusababisha waajiriwa kushindwa kulipwa mafao yao.

“Tayari tumezibaini taasisi mbili na watu binafsi zaidi ya 20 ambao wameshindwa kufanya hivyo na hivyo tunawaomba wengine waweze kuacha tabia hiyo mara moja,” amesema Myava.

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo imeweza kumbana mfanyabiashara mwenye kampuni ya Elgon Traders kuwalipa kkundi cha watu wenye ulemavu bajaji  mbili kati ya tano walizokuwa wanaidai kampuni hiyo baada ya kutoa Sh milioni 36 na kampuni hiyo kushindwa kuwapatia.

“Tunaendelea na mashauri 22 mahakamani ikiwa ni pamoja na mapya mawili ambayo ni dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), mashauri manne, idara ya afya, manne, ardhi shauri moja, Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira(DAWASA) moja, aliyekuwa mtumishi wa wa takukuru moja, wafanyabiashara manne na TANROADS moja, na elimu ya juu moja,” amesema.

Amesema katika kipindi cha Oktoba na Desemba 2020, taasisi hiyo imepokea taarifa 247 kati ya hizo zinazohuru rushwa ni 68, ambapo serikali za mitaa mashauri 16, mahakama 12, polisi saba, elimu sita, ardhi saba, afya tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles