26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi watakiwa kuwa na imani na Serikali

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

JUMUIYA ya Umoja  wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imewatoa hofu Wananchi kwa kuwataka wazidi kuiamini Serikali yao na kuendelea kulipa kodi kwani kila Shilingi inaenda kugusa maisha yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne Agosti 24,2021, Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenan Kihongosi amesema wiki iliyopita Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Mwigulu Nchemba amesema takribani Sh bilioni 48 zimekusanywa na kugawanjwa katika mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vituo 150 vya afya.

“Unapoenda kujenga madarasa unamfanya mtoto wa masikini aweze kusoma.Tunaipongeza Serikali kwani fedha hizo zitaenda kurekebisha barabara na kila Jimbo liliishapewa zaidi ya Sh milioni 500. Uchumi utaenda kuimarika katika maeneo ya vijijini na pato litaongezeka,” amesema Kihongosi.

Hivyo, Kihongosi amewatoa hofu watanzania wazidi kuiamani serikali na kuendelea kulipa kodi kwani kila fedha inaenda kugusa maisha ya watanzania. Hata hivyo, ameiomba serikali fedha hizo ziende zikafanye kazi iliyokusudiwa ili walengwa wazidi kuwa na maendeleo.

“Tunaiomba serikali fedha hizi ziende katika  kazi ile ambayo imekusudiwa wale walengwa husika waende wakaguswe na mambo haya yaweze kwenda vizuri,” amesema Kihongosi.

Katika hatua nyingine,Kihongosi amewataka vijana kuendelea kuchapa kazi, kulipa kodi na kuilinda kwa nguvu zote amani iliyopo ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka.

“Uchumi imara utajengwa na vijana jambo lolote litasimamiwa na vijana wajibu wetu ni kuitii na kuheshimu mamlaka tukisoma historia wazee wetu walifanya kazi kubwa ya kujenga uchumi wetu,sisi wajibu wetu ni kuendeleza mema ili kizazi kinachokuja kitupongeze.

“Nchi hii ilikombolewa na vijana na itasimamiwa na vijana hivyo lazima vijana tulipe kodi kwani wahusika wakuu ni sisi. Niseme sisi kama vijana tutazidi kusimama imara na tutazidi kuhakikisha tunailinda heshima ya nchi yetu viongozi wetu wote kwa sababu tunaamini vijana ndio watu pekee wanaoweza kusema na serikali itakalitekeleza,” amesema Kihongosi.

Kuhusiana na wale wanaoikashfu serikali katika mitandao,Kihongosi amesema: “Nitoe wito nidhamu ni mali na nidamu ni uadilifu, kijana utapimwa unapokosa nidhamu kwa mzazi wako na kiongozi wako maana yake huna tofauti na msaliti lazima tuwe wazalendo tushirikiane na viongozi wetu,”.

Vilevile, amesema hivi karibuni UVCCM itakuja na Programu ya kuandaa makongamano ya fursa pamoja na dira ya jinsi gani ya kutumia vipaji ili kuondokana na changamoto ya ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles