32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA CHAKULA

Na RAMADHAN HASSAN-KONDOA

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Hamza Mafita, amewataka wakazi wa Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma, kuhifadhi chakula ili kiweze kuwasaidia kwa siku zijazo.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Kondoa Mji juzi, Mafita alisema kwa sasa kuna uhaba wa chakula na kwamba njia mojawapo ya kukabiliana na hali hiyo ni wakazi wa Wilaya ya Kondoa kuhifadhi chakula.

“Mwaka huu mavuno si mazuri na mashamba mengi hayajapata mazao, hivyo ni wajibu kwa wananchi wote wa Kondoa, kutunza chakula ili kiweze kuwasaidia kwa siku zijazo.

“Kuna uhaba wa chakula kwa sababu hali ya mavuno mwaka huu si nzuri. Kwa hiyo ninawaomba madiwani wenzangu mkawaambie wananchi wenu watunze chakula angalau magunia 10 kwa msimu.

“Wasisitizieni wafanye hivyo kwa sababu sasa hivi gunia la mahindi ni shilingi 70,000 na bei hiyo inaweza kupanda wakati wowote.

“Pamoja na hayo, madiwani waambieni wananchi wakachukue vitambulisho vya uraia kwani walijitokeza kwa wingi kujiandikisha, lakini hawajaenda kuvichukua katika ofisi za halmashauri.

“Kwa mfano katika Kata ya Mnarani, walijiandikisha zaidi ya watu 400, lakini mpaka sasa waliochukua vitambulisho vyao hawazidi 15,” alisema Mafita.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kolo, Salim Khalifa (CUF), alisema wakazi wa kata yake wamekuwa wakimbana kuhusiana na fidia ya barabara ya Kondoa- Manyara kuwa tathmini walizofanyiwa haziendani na gharama walizojengea nyumba zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles