24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi watakiwa kujenga vituo vya polisi

IGP Mangu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu

NA UPENDO MOSHA, MOSHI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, amewataka wananchi kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi ili kusaidiana na Serikali katika kukabiliana na tatizo la uhalifu nchini.

IGP Mangu alitoa rai hiyo jana mkoani Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Polisi cha Majengo pamoja na jengo la Dawati la  Jinsia na Watoto katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi Mjini,  vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali wa jeshi hilo.

Alisema wananchi hawana budi kuachana na tabia ya kuchoma vituo vya polisi na badala yake waungane na maofisa wa jeshi hilo kuvijenga jambo ambalo ni hatua nzuri katika vita dhidi ya uhalifu nchini.

IGP alisema kuwa uongozi wa jeshi hilo unajitahidi katika kuhakikisha maofisa wake wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.

“Polisi wanapofanya kazi katika mazingira mazuri yasiyo na misukosuko, ni wazi watafanya kazi hizo kwa ufanisi mkubwa huku wakizingatia maadili mema,” alisema.

Aidha alisema kuwa ushirikiano wa wananchi na Jeshi la Polisi kwa dhana ya polisi jamii utalisaidia jeshi hilo kutokana na ukweli kuwa wahalifu wa aina mbalimbali wanaishi mitaani na wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Nchi ya Tanzania kwa sasa ni ya maajabu sana, nasema hivi kwa sababu kila tukio la maendeleo linalopaswa kufanywa ni lazima lifanywe na wananchi. Kila mwezi serikali ya CCM inakusanya kodi kutoka kwa wananchi na vyanzo mbalimbali vya mapato lakini linapokuja suala la maendeleo wananchi hao wanaombwa kuchangia au kujenga maendeleo hayo kwa kutumia vijipesa vyao huku mafisadi wakiendelea kutafuna fedha za walipa kodi. Sasa IGP naye anataka wananchi wajenge vituo vya polisi, je pesa ambazo jeshi la polisi linakusanya kila mwezi kutokana na kutoza faini mbalimbali zinatumika kufanya kazi gani? Shule wajenge wananchi, hospitali na vituo vya afya wajenge wananchi. Swali ni je kati ya wananchi na serikali nani ana kipato kikubwa cha kufanya haya? Jibu lizingatie ukweli kuwa uchumi wa watanzania asilimia 80 unategemea kilimo cha jembe la mkono. Kwa mtindo huu hatutafika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles