24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi walalamikia uhaba wa dawa Ludewa

Na Mwandishi wetu, Njombe

Changamoto ya uhaba wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Ludewa mkoani Njombe imeibua malalamiko miongoni mwa wakazi wa Wilaya hiyo na kusababisha baadhi yao kulalamikia fedha zao za michango ya CHF iliyoboreshwa.

Akizungumza Juzi katika mkutano wa hadhara ya mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga, diwani wa kata ya Ludewa mjini, Monica Mchiro amesema changamoto ya uhaba wa dawa imekuwa ikimpa wakati mgumu kutokana na wananchi wake kumhoji mara kwa mara.

“Kwa kweli wananchi wanalalamika sana watu wanaolipa na wasiolipa wote wanaambiwa wakanunue dawa, mimi nilivyoliona hilo nilifika hospitali na viongozi wa kata kupata taarifa, tuliambiwa kuna vyanzo vitatu vya fedha bima ya afya, CHF na Mfuko wa Basket Fund pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu,” alisema Monica.

Kwa kuliona hilo mbunge, Kamonga amelazimika kufanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ludewa ili kuona uhalisia wa malalamiko hayo ambapo uongozi wa hospitali hiyo chini ya Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Stanley Mlay, umekiri kuwapo kwa changamoto hiyo miezi kadhaa iliyopita tatizo lililosababishwa na ugonjwa wa corona.

“Kulikua na upungufu dawa hapo kipindi cha nyuma lakini tumejitahidi kulitatua kadri ya uwezo kulingana na hali tulioiona dawa za msingi zote zipo wetu na ambazo zimepungua tumejitahidi kuagiza MSD na kuendelea kuongeza makusanyo ili kuona changamoto ya dawa haijitokezi tena,’’amesema Dk. Mlay.

Baadhi ya wagonjwa waliokutwa wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo akiwemo, Elnest Kowi wamesema wamekuwa wakihudumiwa vizuri huku wakiomba huduma kuendelea kuboreshwa zaidi.

Mbunge Kamonga baada ya kutembelea na kukagua hospitali hiyo amejiridhisha na uwepo wa dawa za kutosha huku akiwataka wananchi kuendelea kwenda kupata huduma.

“Kufuatilia changamoto zao kero za wananchi kwenye huduma za afya  ni wajibu wangu tumejitahidi kukusanya Sh bilioni moja, hii ni fedha chache sana inabidi tushirikiane wote kuongeza mapato ili serikali iweze kutoa huduma kwa wananchi waliotuchagua kwa hiyo nimeona hapa kuna dawa za kutosha madaktari wapo na huduma zinaendelea vizuri kwa hiyo niwapongeze na muendelee kuwahudumia wananchi kwa uzalendo moyo na upendo,’’amesema Kamonga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles