24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAILALAMIKIA TANESCO

Na SAFINA SARWATT-MOSHI

WANANCHI zaidi 150 katika Kijiji cha Kigogoni, Kata ya Shirimatunda mkoani Kilimanjaro, wamelilalamikia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani hapa, kwa kushindwa kutatua kero ya umeme ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka mitatu.

Wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni kijijini hapo, wananchi hao walisema tangu mwaka 2,014 hadi sasa, wamekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme kila inapofika saa 12 jioni.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Severen Msele, alisema tatizo hilo limekuwa kero kwao na kwamba wamekuwa wakitumia vibatari ingawa wanatakiwa kuwa na umeme.

“Umeme tumelipia na kuwekewa, lakini usiku tunalazimika kutumia vibatari badala ya umeme. Hili linatuuma sana kwani kila tukipeleka malalamiko yetu huko Tanesco, wamekuwa wakitoa ahadi ambazo hazitekelezeki kwetu.

“Kwa hiyo, hadi tunafikia kuja hapa, tumeanza kuchoka na tumeanza kuona ni bora ieleweke hatuna umeme kuliko kuishi kwa kudanganywa kama watoto,” alisema Msele.

Kwa mujibu wa Msele, tangu mwaka 2014 walipofungiwa umeme, wamekuwa hawafurahii huduma hiyo kwa kuwa kama usipokatika basi unakuwa hauna nguvu ya kuwasha taa.

Akizungumzia malalamiko hayo, Ofisa Habari wa Tanesco, Mkoa wa Kilimanjaro, Samwel Mandare, alisema hawana taarifa ya tatizo hilo ingawa aliahidi kulifuatilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles