25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WANANCHI SINGIDA KUEPUKANA NA KERO YA MAJI

Na MWANDISHI WETU-SINGIDA


WANANCHI wa Kata ya Kinampanda, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, wataondokana na kero ya huduma bora za afya baada ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo kukamilika.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), alipozungumza na wananchi wa kata hiyo jana.

Alisema kwamba, mkandarasi wa ujenzi huo ameshapatikana na Jumatatu ijayo ataanza kazi na kwamba wanatarajia ifikapo mwakani kituo hicho kianze kufanya kazi.

Waziri huyo aliahidi kutoa mifuko 300 ya saruji na nondo 100 za kuanzia, huku akiwataka vijana wajitolee kufyatua matofali.

“Kinampanda ndio ‘centre’ kubwa ya watu wanaotoka maeneo mbalimbali, huduma ikiwa nzuri mtu ataanzia hapa kabla ya kufika Kiomboi.

“Tuna vijiji ambavyo vimezuiwa na mto kwenda Kiomboi, hapa Kinampanda ni karibu zaidi hivyo tuunge mkono ujenzi huu,” alisema Mwigulu.

Alisema kituo hicho kitakuwa na hadhi na ukubwa wa kutosha ambapo kitakuwa na sehemu ya matibabu ya kawaida, kulaza wajawazito na kulaza wagonjwa wengine.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kinampanda, Samwe Kiula, alimshukuru mbunge huyo kwa kuleta ujenzi huo na kuwataka wananchi kuwa tayari kuchangia baadhi ya vitu vitakavyokuwa vinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.

Kwa upande wao vijana wa Iramba wakiwakilishwa na Katibu wa Vijana CCM, Abel Makala, walisema wako tayari kuweka kambi sehemu kunapofanyika ujenzi huo ili kuunga mkono juhudi za ujenzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles