23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Kata ya Ijumbi Muleba wakabiliwa na changamoto ya miundombinu

Na Mwadishi Wetu, Muleba

Wananchi wa Kata ya Ijumbi, Muleba mkoani Kagera wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za miundombinu ikiwamo maji, umeme na elimu kwa kipindi kirefu.

Kata hiyo inakabiliwa na uhaba wa shule za Sekondari kwani iliyopo ni moja inayohudumia wanafunzi 1,070.

Diwani wa Kata Ijumbi, Wilbad Kakuru. akionyesha majengo yaliojengwa na mdau wa maendeleo, Prosper Rweyendera, na kuyakabidhi kwa Serikali ya Kijiji hicho kwa muda mrefu bila kufanyiwa kazi ikiwemo huduma ya afya.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Afisa Mtendaji Kata hiyo, Salehe Mruma na Diwani wa Kata hiyo, Wilbard Musirigi, walipokuwa wakizungumza na Waandishi wa Habari.

Mruma amesema kata hiyo ina vijiji vitano, shule za msingi sita na Sekondari moja ambayo kila mwaka idadi ya wanafunzi inaongezeka na kufanya mahitaji ya vyumba vya madarasa kuwa makubwa.

“Sasa hivi Shule ya Sekondari Ijumbi ina jumla ya wanafunzi 1,070, mwaka huu wanafunzi walioingia kidato cha kwanza ni 342 ambao wanahitaji vyumba saba vya madarasa na wameshajenga viwili.

“Kuna mahitaji ya Sekondari nyingine, majengo, matundu ya vyoo ambayo yanajitajika kila mwaka,”amesema Mruma.

Amesema kwa sasa kuna jumla ya vumba vya madarasa 21 hukunidadi ya wanafunzi ikiwa ni 1,070 na kwamba mwaka huu wamefanikiwa kujenga madarasa mawili ambayo yamesimama yakisubiri kupigwa plasta.

Aidha, amewaonya wanafunzi watoro pamoja na wanaume wanaowapachika mimba wananfunzi.

“Kuna changamoto ya wanafunzi watoro na wengine wanapata mimba, mwaka huu nikimkamata kijana aliyempa mimba mwanafunzi wa darasa la sita nikamkabidhi kwenye vyombo vya sheria,”alisema. 

Upande wake Diwani wa Kata hiyo, Wilbard Musirigi, amesema wanakabiliwa pia na changamoto ya maji ambapo wananchi wanatembea umbali mrefu kufata maji.

Amesema maji kwa wenye uwezo wananunua ndoo moja Sh 300 hadi 400 na ambao hawana uwezo wanayafata kilomita 3 hadi 4 kwenye makorongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles