26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Kagera watakiwa kuondoa hofu chanjo ya corona

Na Renatha Kipaka, Bukoba

WANANCHI mkoani Kagera wametakiwa kuondoa hofu juu ya chanjo ya Covid-19 inayoendelea kutolewa kote nchini ili kujiweka salama.

Kauli hiyo imetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Muhimbili Idara ya Afya ya Jamii, Profesa Deodatus Kakoko, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Bukoba jana kwa lengo la kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa mwananchi.

Profesa Kakoko amesema, Serikali imepanga kufikisha elimu kwa wananchi wengi zaidi kuanzia ngazi ya mtaa ili waweze kupata chanjo sambambana na kuendelea kuchukua hatua za kitaalam.

Amesema kupitia vyombo vya habari vinasikilizwa na wananchi wengi zaidi na kuwa na uwezekanao mkubwa wa hamasa katika kufikisha elimu juu ya madhara ya ugonjwa wa Covid-19 katika jamii.

Aidha, alisema,awali chanajo hiyo ilikuwa ikitolewa kwenye makundi maalum yaliyoelekezwa na wizara lakini sasa yameingizwa makundi ya rika zote.

“Awali chanjo hii ilikuwa kwa makundi maalumu pekee lakini.sasa serikali imekuwa na mpango wa makundi yote kuanzia miaka 18 na kuendekeeaa katika vituo ya kutolea huduma vilivyoanishwa na hospitali za mkoa”amesema Profe. Kakoko

Upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera, Issesanda Kaniki amesema mkoa huo kuna mwitikio mdogo wa wananchi kujitokeza kuchoma chanjo.

Amesema licha ya kuwa na vituo 81 vilivyokuwa vinatoa huduma ya uchanjaji katika Hospitali za Serikali na binafsi lakini bado mwitikio umekuwa hafifu.

Ameongeza kuwa katika mpango huu, ambao umetolewa na Wizara ya Afya wenye lengo la kufikia wananchi wote mkoa huo umeongeza vituo 203 ikiwa ni kurahisisha huduma kwa wananchi.

Hata hivyo amesema katika maeneo ambayo wananchi hupata adha ya kufikia vituo wameweka mpango wa kliniki tembezi ambayo itafiki kila eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles