33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi jimbo la Musoma wampongeza mbunge wao kuhoji gharama za umeme

Na Shomari Binda, Musoma

Wananchi wa jimbo la Musoma mjini mkoani Mara wamepongeza kauli ya mbunge wao, Vedastus Mathayo ya kuomba waraka kuhusu kuunganishiwa huduma ya umeme kwa gharama ya Sh 27,000.

Wakifatilia kikao cha bunge la bajeti katika kipindi cha maswali na majibu katika bunge la bajeti linaloendelea jijini Dodoma, wamesema bado kulikuwa na sintofahamu kuhusu gharama hizo.

Wamesema swali la mbunge wao limekuja wakati muafaka kwa kuwa wamekuwa hawapatiwi majibu mazuri wanapokuwa wanafuatilia kupatiwa na kuunganishiwa huduma.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la, Magesa Juma, amesema alimsikia Waziri wa Nishati akiwa kwenye ziara Musoma juu ya gharama za Sh 27,000 lakini kumekuwa na usumbufu wa kuunganishiwa umeme.

“Tumemsikia mwakilishi wetu bungeni juu ya masuala ya umeme kweli tumekuwa na usumbufu na tunamshukuru kwa kutusemea leo bungeni.

“Tunamuomba mbunge aendelee kufuatilia kwa karibu ili waraka upatikane kwenye ofisi za Tanesco ili watuunganishie umeme kwa gharama nafuu,” amesema Magesa.

Akiuliza swali hilo la nyongeza katika Wizara ya Nishati, mbunge wa jimbo la Musoma mjini, Mathayo alitaka kujua ni lini waraka wa Waziri wa Nishati juu ya wananchi wa jimbo hilo wataungianishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000.

Mathayo amesema Waziri wa Nishati, Medard Kalemani, alipokuwa kwenye ziara mjini Musoma alifanya mkutano wa hadhara na kuwatangazia wananchi wote wa Musoma wataunganishiwa umeme kwa gharama ya Sh 27,000.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, amesema maelekezo ya Waziri ni ya kufanyiwa kazi na wizara itafatilia maelekezo hayo.

Wakati huo huo wananchi wa Musoma mjini wamepongeza Makamu mteule wa Rais Dk. Philip Mpango, kwa kuteuliwa na Rais Samia Suruhu Hassan na kuthibitishwa na Bunge.

Wamesema Mpango ni kiongozi mzuri ambaye kwa mujibu wa wasifu wake atafanya kazi vizuri na Rais Samia katika kuwaletea wananchi maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles