25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanakijiji Makojo waongeza kasi ujenzi wa kituo cha afya

Na Shomari Binda-Musoma

Wananchi wa Kijiji cha Makojo jimbo la Musoma vijijini wameongeza kasi ya nguvu kazi katika ujenzi wa kituo cha afya cha Kata ya Makojo ili kusaidia kukamilika kwa wakati.

Kasi ya wananchi hao imeongezeka katika uchimbaji wa msingi, kusomba mawe, mchanga, matofali na maji kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

Wakizungumza na Mtanzania Digital leo Ijumaa Februari 11, 2022 katika eneo la ujenzi, wananchi hao wamesema wanafanya hivyo kutokana na umuhimu wa huduma za afya.

Wamesema Serikali imeamua kuwaona na kutoa kiasi cha Sh milioni 250 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo hivyo nao ni muhimu kushiriki.

Aidha, licha ya kushiriki, wananchi hao wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali katika huduma za jamii.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mukama Mjinja, amesema kituo hicho cha afya kitakuwa msaada mkubwa kwao katika kupata huduma.

Aidha, amemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kusimama imara kufatilia miradi ya maendeleo.

Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Jimbo la Musoma vijijini kuna ujenzi wa vituo vya afya viwili vya Makojo kinachojengwa kwa fedha za ruzuku ya serikali na kituo cha afya Rukuba kisiwani kinachojengwa kwa fedha za tozo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles