26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WANAOZAGAA TANGA KUKAMATWA

Watendaji Kata na wenyeviti wa mitaa jijini Tanga, wametakiwa kuwakamata wanafunzi watakaoonekana kuzagaa mitaani wakati wa masomo na kuwachukulia hatua wazazi watakaobainika kutofuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni.

Uamuzi huo umetokana na mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika leo Jumanne Januari 16, jijini Tanga ambapo ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo pia ulijadili changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na namna ya kupata ufumbuzi utakaosaidia kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji amewataka walimu wakuu jijini hapa kutowarudisha watoto wenye umri wa kuandikishwa shule kwa kigezo cha kukosa cheti cha kuzaliwa.

“Nawaagiza walimu wakuu kuacha mara moja kuwarudisha watoto kwa kigezo cha cheti cha kuzaliwa badala yake mnapomtilia shaka mtoto watendaji wa kata wapo na wenyeviti waulizwe,” amesema.

Pamoja na mambo mengine kuhusu suala la mimba kwa wanafunzi, mkutano huo umeazimia kuwachulia hatua mwanafunzi atakaemficha aliemtia mimba pamoja na mtiaji mimba ili kudhibiti tatizo la mimba mashuleni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles