SERIKALI KUNUNUA DAWA ZA KUHIFADHI MAITI KWA WAZALISHAJI

0
1170

Serikali inakusudia kuanza kununua dawa za kuhifadhia maiti moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji viwandani ili kupunguza za kuhifadhi maiti katika hospitali mbalimbali nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo leo alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa gharama ya kuhifadhi maiti ambapo itatoa bei elekezi ambayo itakuwa nafuu zaidi.

“Changamoto hii ipo katika maeneo mengi nchini, hivyo tunakusudia kuanza kununua dawa hizi moja kwa moja kwa wazalishaji na kisha tutatoa bei elekezi kwa ajili ya kumpunguzia gharama mwananchi,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here