26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanafunzi, wahitimu wa Afya ya Jamii watakiwa kufanya tafiti za usalama na afya mahali pa kazi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digial

Wanafunzi na wahitimu wa vyuo katika taaluma ya Afya ya Jamii wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo sekta ya utafiti hususan kwenye eneo la usalama na afya mahali pa kazi ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mlezi wa wanafunzi wanaosoma masomo ya afya ya jamii na sayansi shirikishi katika chuo kikuu MUHIMBILI, Prof. Gastro Frumence akihamasisha wanafunzi na wadau mbalimbali waliohudhuria katika jukwaa la kwanza la Sayansi ya Afya ya Jamii na Mazingira kuongeza ubunifu katika tafiti wanazozifanya ili zilete tija katika jamii na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo wanaosoma masomo ya Afya ya Mazingira nchini(TEHSA), Dk. Hussein Mohamed katika Jukwaa la kwanza la Sayansi ya Afya ya Jamii na Mazingira lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo, wahadhiri pamoja na wabobozi wa utafiti kutoka maeneo mbalimbali nchini ili kubadilishana uzoefu, elimu pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta hizo.

“Kuna fursa nyingi sana katika sekta hii ya afya ya mazingira kinachotakiwa ni mtafiti mwenyewe kuangalia tatizo liko wapi ili aweze kufanyia utafiti mfano anaweza kuamua kufanya utafiti wa kubaini vihatarishi vilivyopo katika maeneo ya kazi na zaidi tafiti hizi hazipo kwa ajili ya kumsaidia mwanafunzi kumaliza Shahada yake bali zinaweza kutumika kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, hivyo nitoe wito kwa wanafunzi na watafiti wote kuchangamkia fursa hii,” amesema Dk. Mohamed.

Mkufunzi wa mafunzo wa OSHA, Imakulata Longino akiwasilisha mada mbalimbali za usalama na afya mahali pa kazi kwa wanafunzi na wadau waliojitokeza katika jukwaa la Sayansi ya Afya ya Jamii na Mazingira.

Kupitia jukwaa hilo lililofadhiliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili wakishirikiana na Jumuiya ya wanafunzi wanaosoma masomo ya afya ya mazingira nchini, OSHA imewasilisha mada mbalimbali ikiwemo elimu juu ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi pamoja na kuwajengea uelewa wanafunzi hao juu ya namna ya kutambua fursa mbalimbali watakapo hitimu vyuo.

“Baada ya kutoa mafunzo haya tunatarajia wanafunzi hawa watakuwa na uelewa mkubwa wa kutambua fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuhamasika kufanya tafiti katika maeneo ya kazi na tafiti hizo tunaamini zinaweza kusaidia maeneo ya kazi, jamii na hata taasisi yetu kwa ujumla,” amesema Imakulata Longino Mkufunzi wa mafunzo wa OSHA.

Kwa upande wake Mlezi wa wanafunzi wanaosoma kada ya afya ya umma na sayansi shirikishi katika Chuo kikuu Muhimbili pamoja na Rais wa Jumuiya ya TEHSA wameishukuru OSHA kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha jukwaa hilo huku wakitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono.

“Tunawashukuru sana OSHA kwasababu wamekuwa ni wadau wetu wakubwa sana katika kuwashika mkono wanafunzi wetu wa kada ya afya ya mazingira na si kwa mwaka huu tu bali hata majukwaa mangine yaliyopita walituunga mkono hivyo nitoe wito wangu kwa OSHA na wadau wengine kuendelea kutuunga mkono katika masula mbalimbali kwa sababu wanafunzi hawa ni wadau wenu wakubwa pia,” amesema Prof. Gastro Frumence ambaye ni mlezi wa wanafunzi wa kada ya afya ya umma na sayansi shirikishi Muhimbili.

“Kupitia OSHA tumeweka kuandaa jukwaa hili kubwa la kitaifa lililowakutanisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini na tumepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia jukwaa hili ikiwemo elimu ya masuala ya usalama na afya kazini lakini pia fursa zilizopo katika sekta ya utafiti hivyo tunawashukuru san ana tunawaomba muondelee kutuunga mkono,” amesema Rais wa TEHSA, Raphael Alphonce.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mijadala na tafiti mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa jukwaa la kwanza la Sayansi ya Afya ya Jamii na Mazingira lilofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi MIHIMBILI.

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili kikishirikiana na Jumuiya ya umoja wa wanafunzi wa vyuo wanaosoma kada ya afya ya mazingira nchini-TEHSA wamekuwa wakiandaa majukwaa mbalimbali kwa lengo la kukuza taaluma kwa wanafunzi hao kwa kuwakutanisha na wataalam mbalimbali ilikubadilishana uzoefu,elimu na fursa katika maeneo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles