25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI HUTEGEMEA MITANDAO KUFANYA KAZI ZA CHUO

Na Joseph Lino


‘COPY and Paste’ hili limekuwa neno la kawaida kwa wanafunzi wa chuo ambapo wengi hutumia mbinu hiyo kurahisisha kazi aliyopewa na mwalimu.

Copy na Paste (Kuiga na Weka) humaanisha kuchukua na kuweka kazi iliyoandikwa na mtu mwingine kama ilivyo bila ruhusa au kibali cha mhusika.

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha DePaul nchini Marekani aliiga aya (paragraph) kutoka  kwenye mtandao na kuweka katika utafiti (research) na kuwasilisha bila matatizo kwa msimamizi wake. Lakini baadae msimamizi aligundua aya hiyo, kwamba mwanafunzi aliichukua kutoka kwenye mtandao hivyo kumsababishia kupunguziwa alama za ufaulu.

Ingawa vyuo vingi hufuatilia kanuni za uendeshaji na mahitaji ya kozi kuhusiana masuala kuiga kazi kwa kuwa ni kinyume na sheria, lakini tabia hiyo inazidi kuongezeka katika ulimwengu wa mtandao wa intaneti.

Kukosekana kwa mawasiliano kati ya wanafunzi na vyuo kumesababisha kuwapo kwa ongezeko la wanafunzi wanaoiga kazi ya mtu mwingine na kuifanya kama ya kwake (plagiarism).

Mtandao wa Education Lawyers unaelezea namna matumizi ya mtandao hutoa fursa kwa wanafunzi kupata vyanzo vya tafiti na taarifa mbalimbali tofauti na miaka ya nyuma.

Vitendo vya kuiga kazi na kuhaririwa vizuri ili kuondoa maneno yasiyofaa ni juhudi ambazo mwanafunzi anafanya kila wakati.

Baadhi ya wanafunzi wa leo huwa wanakamilisha kazi ambayo aya nyingi zimechukuliwa katika intaneti bila kutoa shukurani kwa chanzo chake.

Mtandao huo unaeleza kuwa wanafunzi wanaweza kuchanganyikiwa wasijue namna wanavyopaswa kutoa shukurani kwa chanzo cha intaneti katika kazi za chuo.

Mwanzilishi wa Kituo cha Academic Intergrity wa Chuo Kikuu cha Rutgers nchini Marekani, Profesa Donald Mccabe  aliendesha utafiti kwa wanafunzi kuhusiana na copy na paste.

Utafiti waMcCabe  ulionesha kuwa asilimia 40 ya wanafunzi 14,000 wa shahada ya kwanza walikubali kuiga aya kutoka vyanzo vingine katika kazi zao walizopewa na mwalimu kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.

Wanafunzi wachache wanaona kuiga baadhi ya aya kutoka mitandaoni ni udanganyifu mkubwa.

Pia kuna tofauti kubwa ya kizazi kilichopo na cha miaka ya nyuma ya wanafunzi vijana na wenye umri mkubwa.

Wanafunzi vijana na wanafunzi wa zamani, hutazama maadili ya kitaaluma kwa mrengo tofauti. Makundi haya mawili hawaoni tofauti ya kazi halisi kwa mtazamo mmoja.

Wanafunzi vijana huwa na kiwango kikubwa cha faraja katika kutafuta kazi ya kuiga katika vyanzo mbalimbali pindi wanapofanya utafiti.

Wanafunzi wengi na walimu huwa na wasiwasi wakati wa kutoa alama sahihi kwa kazi ambayo vyanzo vyake ni mitandao.

Kwa upande mwingine, vyuo huwa na sera dhidi ya kudanganya au kuiga kwenye tovuti ya chuo, vitabu vya wanafunzi kuhusu kanuni za nidhamu zinazofafanua masuala ya kuiga, kudanganya na hasara ya ukiukwaji wa vitendo hivyo.

Matokeo ya kuiga kazi katika mitandao yanaweza kusababisha kusimamishwa chuo kwa muda au kufukuzwa kabisa.

Makosa madogo yanaweza kuathiri alama za ufaulu kwa mwanafunzi au kuondolewa darasani.

Kwa mujibu wa  mtandao huo, hakuna kitu kibaya kwa mwanafunzi kufanya juhudi za maendeleo ya kitaaluma, lakini juhudi za hazipaswi kusababisha kuiga kazi isiyo yake.

Wanafunzi na walimu wanahitaji kuchukua hatua ili kuhakikisha wanafunzi wanafanya kazi zao wenyewe na si kuchukua sifa kutoka kwa watu wengine.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles