28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 68 wapata ujauzito Maswa

Na Derick Milton, Maswa.

Jumla ya wanafunzi 68 kutoka shule za msingi na Sekondari katika Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu wamepata ujauzito katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu na kusababisa kukatisha ndoto zao.

Taarifa ya jeshi la polisi Wilayani humo kutoka Dawati la jinsia, imeeleza kuwa kwa shule za msingi ni wanafunzi watatu huku sekondari wakiwa wanafunzi 65.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa Dawati hilo Anande Masai wakati wa kilele cha maazimisho ya siku 16 za kupiga vita ukatili wa kijinsia Wilayani humo yaliyofanyika kijiji cha Shishiyu yaliyoratibiwa na Shirika la Worldvison Tanzania.

Maandamano ya wanafunzi na wanawake katika Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, wakati wa kilele cha maazimisho ya siku 16 ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika Kijiji cha Shishiyu Wilayani humo na kuratibiwa na Shirika la Worldvison Tanzania.

WP Anande Amesema kuwa jumla ya kesi 27 zilihusu mimba za wanafunzi hao, ndizo zilifikishwa mahakamani, ambapo nane kati ya hizo zimetolewa hukumu, 10 zinaendelea kusikilizwa na 6 zimeondolewa Mahakani.

Amesema kuwa jamii bado imeendelea kuficha taarifa za matukio hayo ya mimba kwa wanafunzi kwa kumalizana kienyeji, ikiwa pamoja na kushindwa kutoa ushahidi mahakamani kwa baadhi ya kesi ambazo zipo katika chombo hicho cha haki.

Mbali na mimba Anande amesema kuwa katika Dawati hilo wamepokea matukio 148 ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na matukio 195 kwa watu wazima wakiwemo wanaume 20 kwenye Wilaya hiyo.

Akizungumza kwenye maazimisho hayo Mratibu wa Worldvison Tanzania Mradi wa maendeleo ya jamii Shishiyu Yohana Masanja amewataka wadau wote kuungana kwa pamoja katika kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kwenye jamii.

Aidha Masanja amesema kuwa elimu endelevu kwa jamii inatakiwa kila wakati katika kuhakikisha inatambua haki za kila mtu, ikiwa pamoja na kuondokana na mitazamo hasi, imani au desturi ambazo zimepitwa na wakati.

“Kampeini ya kupinga vita vitendo hivi inatakiwa kutolewa kwa makundi mbalimbali ya jamii Kama vile viongozi wa dini, vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi,” amesema Masanja.

Kwa upande wake Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya hiyo Fredrick Lukuna aliwataka wazazi na walezi kuacha kukwepa majukumu yao kulea watoto.

” Siku hizi wawazi na walezi wamewaachia walimu kulea watoto wao, hawataki kubeba majukumu yao kama wazazi, wamewaachia watu wengine ambao ndiyo wamekuwa wakiwafanyia vitendo hivi watoto na kuwapa mimba,” amesema Lukuna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles