25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 500,000 wahitimu VETA

wanafunzi VETA
wanafunzi VETA

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI zaidi ya 500,000 wamehitimu kozi mbalimbali katika vyuo vya Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) tangu vyuo hivyo vilipoanzishwa nchini mwaka 1996.

Akizungumza na MTANZANIA katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Mtafiti wa Masoko ya Kazi, Makao Makuu ya VETA Dar es Salaam, Julius Mjelwa, alisema wanafunzi hao ni waliosoma kozi fupi na kozi ndefu.

Alisema kutokana na idadi hiyo, mwaka 2010 walifanya utafiti kujua kama wahitimu wameajiriwa au wamejiajiri na kugundua kuwa asilimia 66 wameajiriwa katika sekta mbalimbali.

“Pamoja na utafiti huo, mwaka jana tulifanya utafiti mdogo ili kujua kama waliosoma mambo ya ujasiriamali na ufundi wameajiriwa au hawakuajiriwa.

“Katika utafiti huo, tuligundua wanafunzi wetu zaidi ya asilimia 77 wameajiriwa na kujiajiri jambo ambalo ni la kujivunia,” alisema Mjelwa.

Pamoja na hayo aliwataka wahitimu wote wa VETA watumie ujuzi wao katika masuala mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wenzao wasiojua umuhimu wa VETA.

“Wahitimu wote ni bora wakatumia ujuzi tuliowapa katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo, kwa sababu ujuzi huo utasaidia katika kukuza uchumi wa taifa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles