29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki maduka dawa za binadamu wapewa onyo

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

MSAJILI wa Baraza la Famasi Tanzania,Elizabeth Shekalaghe,  imewapa onyo  wamiliki  wa maduka ya dawa  za binadamu kuacha kuweka  matangazo ya huduma katika milango ya maduka yao kwani ni kinyume na Sheria ya  baraza hilo, huku akisema watakaokiuka watafungiwa  kutoa huduma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo  Desemba 10,2021,kuhusu matumizi holela ya dawa, ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kununua dawa kiholela kwani ni sumu na huleta madhara pale mtu anapotumia bila kufuata ushauri wa wataalamu.

“Kumekuwa na utaratibu watu kuweka mabango kwenye milango kana kwamba wanatoa matibabu au anaweka picha ya daktari kwamba tunatoa  ushauri kama kuna huduma zinapatikana

“Niwaombe wamiliki wa maduka ya madawa kuacha mara moja na ndugu zangu nitakapopita na kukuta unatangaza, kisheria tunatakiwa kukufungia huduma,”amesema.

Aidha, amewataka  wafamasia ambao hawajahuisha  leseni zao kufanya hivyo kabla ya Desemba 31,2021 kupitia mfumo wa kielektroniki.

“Sheria inawataka wanataaluma wote kufanya marejeo ya leseni zetu kwa mwaka sasa hivi tupo katika hatua nzuri kwani kati ya wafamasia 2597 ambao wamesajiliwa 2479 wamehuisha leseni zao sawa na asilimia 93,”amesema.

“Ni vema wananchi  mkafahamu kuwa zipo athari za matumizi yasiyo sahihi  ya dawa na athari zake ni kuongezeka kwa ugonjwa,kutokupata nafuu,kutokupona na hatimaye kupelekea kifo,”amesema.

Amewataka wananchi kuepuka kununua dawa kwenye maduka ambayo hayajasajiliwa  na Baraza la Famasi kwani ubora wake ni wa mashaka  na maelezo juu ya dawa hizo yanaweza kupotoshwa.

Pia  amewataka  wafamasia,mafundi sanifu wa dawa na wasimamizi kuzingatia sheria.

“Wafamasia wenzangu tuhakikishe tunasimamia  misingi ya utoaji huduma kwenye  taaluma hii ambayo tumeisomea,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles