24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waliopona corona nchini sasa watano, Arusha hakuna mgonjwa

AVELINE KITOMARY Na BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema wagonjwa wengine wawili waliokuwa na virusi vya Corona  (Covid-19), wamepona na kurudi nyumbani huku akiwahasa wananchi kutowanyanyapaa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ummy, alisema kufikia sasa idadi ya watu waliopona virusi hivyo nchini ni watano, huku mmoja kiwa amefariki dunia ambao walikuwa Dar es Salaam na  Arusha.

Alisema takwimu za jana kutoka maabara zinaonesha hakuna maambukizi mapya ya virusi vya  Corona.

“Hatuna maambukizi mapya, wenye maambukizi wanabaki 24 na wawili wameshapona (aliowatangaza jana) aliyeko Dar es Salaam tumemruhusu wa Arusha pia  tume mruhusu, Arusha  hatuna mgonjwa, tumebakiwa na Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar.

“Waliopona maambukizi tunatakiwa kuwapokea na sio kuwanyanyapaa, tumeshawapa elimu, waendelee kujitunza na kujikinga na maambukizi, kwa sababu kuna takwimu tumezipata kutoka China, zinaonyesha katika kila watu 100 waliopona, 14 wanaweza kuambukizwa tena,”alisema.

Alisema pia Serikali haina mchezo na suala la karantini, hivyo wageni wote kutoka nje watalala katika hostel za Magufuli zilizoko Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Tunatambua zipo changamoto, tutazitatua lakini hakuna mbadala wa mtu yoyote kutoka kwenye hosteli hizi” alisema Ummy.

Aidha aliwataka Watanzania  kujitahidi kuepuka mikusanyiko na kukaa umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine ili kuzuia maambukizi.

Katika hatua nyingine Ummy alipokea vifaa mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

“Tumepokea madumu ya kunawa mikono, (simtanki) 1,000 kutoka kwa Subhash Patel, kupitia umoja wa wafanyabiashara wazalendo ambao waliahidi kwa Waziri Mkuu na sasa wametimiza”

“Namkabithi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam madumu ya kunawia mikono, 350 na mengine 650 yatapelekwa kila mkoa utapata 26, kwa Dar es Salaam, tumeona maambukizi ni mengi na kwa kuwa wanasehemu nyingi za wazi uhitaji ni mkubwa”alisema Ummy.

Kwa upande wa  Makonda aliwashukuru wafanyabiashara hao kutoka msaada huo kwa watanzania.

“Nawashukuru viongozi wa dini wanaoendelea kuombea nchi yetu na takwimu zinaonyesha tupo kwenye 24 wakati nchi zingine zinahangaika na Mungu tumeona akitutetea na kutujibu,” alisema.

Alisema pia wasafiri walio kwenye Hostel za Magufuli si masikini, ila hatua hiyo imefikiwa baada ya kupewa uhuru wa kukaa hiotelini na kuutumia vibaya kwa kuzurura kwenye mabaa na kumbi za starehe.

Aliwataka wakurugenzi wote wa manispaa za jiji hilo kuhakikisha maji yenye dawa hayamaliziki kwenye ndoo ya kunawia mikono.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara Subhash Patel, alisema huu ni wakati wa kila Mtanzania mwenye uwezo kusaidia asiye jiweza.

“Tutaendelea kutengeneza na kusaidia wengine vitu hivyo vinathamani ya Sh milioni 300 za kitanzania.

CTI kufanya tathimini adhari ya corona

Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) limesema linafanya tathmini kujua namna ambavyo viwanda vimeathiriwa kutokana na kuwapo kwa janga hilo.

Akizungumza na MTANZANIA, Mtaalamu wa Sera wa CTI, Frank Dafa, alisema baadhi ya wanachama wao wameathiriwa na janga hilo ndiyo maana wameamua kufanya tathmini ya jumla kujua ukubwa wa tatizo. 

“Tunafanya ‘survey’ kwa sababu tuna taarifa za mmoja mmoja, bado hatujapata ‘position ya organization’, wengi wameanza kusema imewa – affect.

“Hatari tunayoiona ni kuishiwa malighafi mfano kutoka India au China na inaweza kusababisha baadhi ya viwanda vikafungwa au kupunguza ‘shift’ kwa sababu ‘stock’ zinaisha,” anasema Dafa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles