25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Ahadi ya Rais Magufuli kuwapa pikipiki maofisa tarafa yatimizwa

Benjamin Masese -Mwanza

RAIS Dk. John Magufuli amewakabidhi pikipiki 24 maofisa tarafa wa Mkoa wa Mwanza zenye thamani ya Sh milioni 48 kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya Rais Magufuli, alisema zimetolewa ikiwa ni utekeleaji wa ahadi yake aliyoitoa Juni 4 mwaka jana alipokutana na maofisa hao Ikulu Dar es Salaam katika kikao cha pamoja  kilichowajumuisha  makatibu tawala wa wilaya nchini nzima.

Alisema katika Mkoa wa Mwanza kuna maofisa tawala 24 katika wilaya saba za mkoa huo na katika Wilaya ya Kwimba walikabidhiwa pikipiki tano, Sengerema (5), Magu (4), Misungwi (4), Ukerewe (4), Ilemela (1) na Nyamagana (1).

“Hizi pikipiki 24 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Magufuli. Kama mtakumbuka Juni 4 mwaka jana  alikutana na maofisa tarafa na makatibu tawala wa wilaya nchi nzima ambapo katika mazungumzo yao walimweleza wana changamoto ya usafiri wa kuwafikia wananchi ukizingatia tarafa moja inaweza kuwa na vijiji  10 au zaidi.

“Ahadi ya Rais Magufuli ilitimizwa rasmi Machi 18, mwaka huu ambapo pikipiki za maofisa tarafa nchi nzima zilikabidhiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejienti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-Tamisemi), George Mkuchika, hivyo zimesambazwa kila mkoa ili nasi kama wakuu wa mikoa tuzikabidhi kwa niaba yake.

“Sasa pikipiki hizi zimeletwa kwa ajili ya maofisa tarafa kwa ajili ya kusimamia usalama, kuhamasisha na kukagua  shughuli za maendeleo, sitegemei kuona au kusikia vyombo hivi ambavyo ni mkono wa Rais Magufuli vikiwa vijiweni vikifanya kazi ya kusafirisha abiria, hatua kali zitachukuliwa na kibarua chako kitakuwa hatarini,” alisema Mongela.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles