29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu wahamishwa kwa nguvu Mwanza

Na Sheila Katikula, Mwanza

Halmshauri ya Jiji la Mwanza imewahamisha kwa nguvu kwenye nyumba walizokuwa wanakaa walimu wanne wa shule za sekondari Mlimani, Mapango na Pamba za Jiji hilo ili kupisha ukarabati unaotekelezwa na Serikali.

Zoezi  la kuwaondoa walimu hao kwenye nyumba hizo limefanyika baada ya kukataa kuhama kwa hiari na kudai hawajalipwa fedha za kufunga mizigo. Zoezi hilo limefanyika kwa kusimamiwa na askari mgambo.

Akisimamia zoezi hilo jana kwa niaba Mkurugenzi wa Jiji, Kiomoni Kibamba, Ofisa Mtendaji wa kata ya pamba, Jonas Mugisha  amesema walimu hao wameondolewa kwa nguvu  baada ya  kukaidi amri ya kuhama  kwa hiari kupisha ukarabati wa nyumba hizo.

Amesema walimu hao walipewa barua iliyokuwa ikiwataka kuhama   kwenye nyumba hizo ili ziweze kukarabatiwa pamoja na shule hiyo kwani serikali imetowa Sh milioni 540.

Mmoja wa walimu hao, Abel Dendwa akizungumza kwa niaba ya walimu hao amesema inasikitisha kuona mfanyakazi wa umma anafanyiwa vitendo vya unyanyasaji nakwamba ni vema serikali ikaingilia kati suala hilo ili haki iweze kutendeka ikiwamo ya kulipwa fedha zao za kufunga mizigo.

“Pamba sekondari walikataa na kuhamishiwa milimani Sekondari lakini fedha za kufunga mizingo sijapewa sasa ninavyopewa barua ya iliyokuwa inanitaka nihame na haki yangu sijapewa ndiyo maana tumekataa,” amesema Dendwa.

Amesema inasikitisha kuona mfanyakazi wa umma ananyanyaswa  ni vema serikali kuingilia kati suala hilo ili haki iweze kutendeka ikiwemo kulipwa stahiki zao.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Nyamagana (CWT), Sholi Maduhu, amesema hana taarifa yoyote kuhusu walimu hao zoezi  hilo la uzalilishaji kuwaondoa kwa nguvu walimu hao.

“Nimelishudia zoezi hili siwezi kuzungumza chochote kwa sababu  sina taarifa nitafatilia Kwa Mkurugenzi  ili niweze kujilizisha ndiyo nitatoa  tamko,” amesema Maduhu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba amesema kuwa walimu hao niajambazi  kwa sababu  fedha za kufunga mizigo walishalipwa lakini bado wang’ang’ania kwenye nyumba hizo .

Alisema  nyumba kwa walimu siyo haki yao ila ni hisani tu Kwa Serikali kuna  utaratibu ukipewa zamana fulani  inayostahili  kupewa kuna viti unaandilkiwa  kwenye barua yako pindi unapoajiriwa. 

Alisema kwa waliohamia mbali walilipwa fedha zao ila kwa walimu aliyehamia karibu hana sifa za kupewa hela za kufunga mizigo.

“Walimu hawatayari  wameshalipwa fedha za kufunga mzigo ila mwalimu mmoja h ana sifa za kupata posho hiyo k wa asababu litoka Mwanza Sekondali na kuhamia Shule ya jirani.

“Septemba,mwaka jana Serikali ilitoa fedha hizo kwa ajiri ya ukarabati wa   Shule mabweni, madarasa na   nyumba za walimu 13 lakini walimu hawa nilishawapa barua za  kupisha ujenzi lakini wamekataa ndiyo maana tumeamua kutumia nguvu. 

“Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo aliwaita mwezi Septamba mwaka jana na kuwapa taarifa ya ukarabati huo na kuwaomba wapishe zoezi hilo   wakimaliza ujenzi huo watarudi kwani nyumba tisa walimu walihama kwa hiari ila hizi  nne ndiyo kuna changamoto,” alisema Kibamba

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles