Na Safina Sarwatt, Moshi
Walimu saba katika shule ya msingi mikocheni iliyopo kata ya Arusha chini wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wanalazimika kuishi nyumba moja yenye vyumba vitatu ambapo kati yao wakike wanne na wanaume wanaume watatu.
Walimu hao wakizungumza na MtanzaniaDigital shuleni hapo leo Januari 20, 2021 wamesema wanafanyakazi katika mazingira magumu huku familia zao zikiishi Boma Ng’ombe wilayani Hai njia panda ya Himo.
Mmoja wa walimu hao, Melkizedick Temba amesema mazingira hayo yamesababisha walimu kushindwa kufanya kazi kwa weledi .
Amesema nyumba hiyo haina choo wala bafu na kwamba wanalazimika kutumia vyoo vya wanafunzi.
Amesema vyumba vya madarasa pia hayatoshelezi wanalazimika kufundisha wanafunzi zaidi ya 170 kwenye chumba kimoja na kwamba mwalimu anashindwa kuwafikia kwa wakati moja wanafunzi wote.