24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu Dodoma watakiwa kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Fatma Mganga, amewataka walimu wanawake wa mkoani humo kuwasaidia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao darasa la saba na kidato cha nne ambapo amedai kitaalum mkoa huo umekuwa haufanyi vizuri.

Pia amewataka kuwa na maadili katika utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kusimamia maadili na mavazi ya walimu kwani baadhi wamekuwa wakivaa mavazi mafupi na ambayo hayana stara katika jamii.

Akizungumza Desemba 3, katika Kongamano la Wajumbe kutoka Kitengo cha Walimu wanawake Mkoa wa Dodoma liloandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Katibu Tawala huyo amesema hali ya taalumu katika mkoani humo sio nzuri hivyo amewaomba walimu hao wanawake wamsaidie ili ndoto yake ya kufanya vizuri iweze kutimia.

Katika kongamano hilo kuliwasilishwa mada mbili ambazo ni ujasiriamali pamoja na Maadili ya utumishi wa umma  mahala pa kazi.

“Tuna mpango wa Dodoma kuingia katika kumi bora lakini sisi peke yetu hatuwezi hapa niongee nanyi kama walimu lakini pia kama wanawake, wanawake kwanza hawapendi kushindwa ninaomba jambo letu la taaluma tuliangalie.

“Jamani ninaomba niwaombe tujitahidi kwa nguvu zote kwa akili zote kwa maarifa yote na inawezekana ni  Commitment tu,”amesema.

Pia, amewataka walimu hao wanawake kuzingatia maadili kwani walimu ni kioo cha jamii ambapo amedai kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakivaa mavazi ambayo hajakubaliki katika jamii.

“Walimu ni kioo cha jamii Mwalimu unavaa kinguo unamtega nani unamtega mwanafunzi?hawa walimu wapya tukawafundishe ili tuwatengeneze wanawake wa kesho,”amesema.

Vilevile amewataka viongozi hao kuleta mabadiliko katika kila ambacho wanakifanya huku akisisitiza usimamizi wao uwe ni wa mfano.

“Sasa wanawake ndio tumekabidhiwa Nchi hivyo kwa nafasi yoyote onesha kwamba unaweza uongozi ni dhamana tunawajibu wa kubadilisha mambo kiongozi asieleta mabadiliko huyo sio kiongozi,”amesema.

Katibu Tawala huyo pia amewataka walimu wanawake hao, kujitegemea kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutokukopa mikopo ambayo ni umiza.

“Nendeni mkatunze mazingira wanawake tunapaswa kutunza mazingira niwaombe tukapande miti katika maeneo ya shule,”amesema.

Kwa upande wake,Mwenyekiti Kitengo cha Wanawake walimu Mkoa wa Dodoma, Eliakumburusa Elias amewataka walimu kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuacha alama katika utendaji kazi wao.

Vilevile amewataka kujiendeleza kielimu,kusimamia maadili hasa ya walimu wapya ambao wamekuwa wakiajiriwa ,pamoja na kuweka vizuri maeneo yao ya kufanyia kazi.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Dodoma, Samweli Malecela amesema anaamini dunia ipo katika mikono salama kutokana na uwepo wa wanawake huku akisisitiza kwamba kina mama ni waaminifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles