Anjapaly, Madagascar
Mkurugenzi wa Shirika la mpango wa chakula duniani David Beasley, amesema mji wa kusini mwa Madagascar unaokubwa na njaa pamoja na ukame kwa muda wa miongo minne linaitaji msaada wa haraka.
Beasley, ambaye amefanya ziara katika mji huo amesema watu zaidi ya nusu milioni wanaitaji msaada wa haraka pia ameongozea na kusema kuwa alishitushwa na kile alichokiona Kusini mwa Madagascar ambako watoto walikuwa wamebakia tu na mifupa yenye ngozi, na familia zilikuwa zikila matope na matunda pori kwasababu hapakuwa na kitu kingine.
Beasley ameiita hali inayoendelea katika kusini mwa Madagascar ‘’janga la kimya lililo katika eneo lilililosahahulika.
Hata hivyo mzozo huo unasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo ukame umeendelea kuwepo na kuzilazimisha familia kuzihama nyumba zao.
Amesema kuwa mataifa tajiri hayana maadili ya uwajibikaji kwa kutoa msaada.