31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge la Uganda la fungwa

Kampala, Uganda

Bunge la Nchini Uganda linatarajiwa kufungwa kuanzia Juni 28, 2021 kwa muda wa wiki mbili hadi Julai 11, 2021 kwaajili ya kusafisha majengo ya bunge hilo dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasilianona masuala ya umma katika bunge hilo, Chris Obore amesema uamuzi huo ulichukuliwa ili kuzuia jengo hilo kuwa kitovu cha maambukizi kwasababu ya idadi kubwa ya watu wanaolitembelea.

Bunge la sasa la Uganda lina jumla ya wabunge 529 , ukiondoa wahudumu wa bunge, maafisa wa usalama, waandishi wa habari, na watoaji wa huduma mbalimbali.

Taasisi hiyo ilikuwa na matukio muhimu makuu tangu mwezi Mei miongoni mwake ikiwa ni kusomwa kwa bajeti, na Hotuba ya hali ya taifa ambayo hutolewa na rais.

Mamia ambao walihudhuria matukio hayo wametakiwa kufanya vipimo vya corona huku watakao patikana na maambukizi watatakiwa  kujitenga wenyewe.

Takriban watu 180 walipatikana na maambukizi ya corona kabla ya matukio haya mawili tofauti  huku 14 kati yao walikuwa ni wabunge na 10 walikuwa ni wafanyakazi wa bunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles