25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WATAKIWA KUPIMA AFYA YA UDONGO

 

 

Na MWANDISHI WETU, MBEYA


TAASISI ya Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini  mwa Tanzania (SAGCOT),  imesema licha ya wakulima kuitikia wito wa kutumia mbegu bora na mbolea, lakini kukosekana  maarifa ya kutunza udongo ili kustawisha mazao shambani ndiyo sababu mojawapo iliyosababisha  kilimo chenye kuleta tija ya uzalishaji kushuka.

Akizungumza   Mbeya jana, Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga,  alisema wakati umefika kwa wakulima katika ngazi zote kujenga tabia ya kupima afya ya udongo ili kuongeza tija na uzalishaji zaidi katika kilimo.

“Wakulima wameitikia wito wa kutumia mbegu bora na mbolea lakini kitu ambacho kinakosekana ni maarifa ya kutunza udongo.

“Kwa hivyo kuna haja ya kupima udongo na kujua afya yake ikoje kwa sababu kama usipozingatia hilo huwezi kupata zile tija ambazo zitaleta mageuzi ya kumtoa mkulima kwenye  hali ya umasikini,” alisema Kirenga.

Alikuwa akizungumza  kwenye Maonyesho ya Wakulima Nanenane  yanayoendelea jijini hapa ambako SAGCOT imeweza kuwakutanisha wafanyabiashara na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwenye sekta ya kilimo  na kusimamia sheria na utaratibu.

Kirenga alisema kuna haja ya kupima  afya ya udongo  kuleta tija itakayosaidia kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo nchini.

Alisema mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni kapu la uzalishaji wa chakula  nchini ambako kwa wastani inazalisha chakula kwa asilimia 60 hadi 65 ya mazao yote yanayoliwa  nchini.

Kirenga alisema  ndiyo maana Sagcot imekuwa ikishirikiana na wabia  na teknolojia kuona wanavyoweza kuleta mageuzi ya kilimo.

“Ni eneo ambalo lina hewa na udongo wake mzuri, mvua inapatikana kwa uhakika kuliko maeneo mengine, kuna wananchi ambao ni wachapa kazi wakiwamo vijana nakina mama wanaojituma kwa wingi sana.

“Lakini elimu bila maarifa haikupi matokeo yale ambayo ulikuwa unastahili kupata,” alisema Kirenga.

Alisema wastani wa tija na uzalishaji wa mazao katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni kati ya tani 1.3 kwenye   mahindi mpaka tani tatu.

“Likini wale wakulima ambao wamefuata sheria, taratibu na kanuni za kilimo bora za kilimo hasa wale wameangalia masuala ya afya ya udongo, tija inaweza ikatoka kwenye hiyo tani tatu  ikafika mpaka tani 13 kwa hekta,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mpango wa pilli wa Serikali wa kuendeleza sekta ya kilimo nchini (SPD2), Kirenga alisema mpango huo utaweza kuleta mageuzi Serikali itakapoamua kushirikiana na sekta binafsi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles