27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa kahawa nchini watakiwa kuongeza tija

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amewataka wakulima wa Kahawa nchini kulima zao hilo kwa kuliongezea tija.

Hayo aliyasema hivi karibuni wakati alipokuwa akizungumza katika maonyesho ya 45 ya Sabasaba, ambako alisema hivi sasa Serikali imejikita kupiga kampeni ya kila zao kama vile Kahawa, Pamba, Korosho, Tumbaku, Zabibu na mengine.

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda (wa nne kutoka upande wa kulia) na Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo (wa tatu toka upande wa kushoto) wakionja ubora wa Kahawa wakati wa uzinduzi wa siku maaum ya Kahawa kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, maonesho hayo yalianza Juni 28 na yanatarajia kimalizika Julai 13 Mwaka huu.

Alisema, “Kila tunapokwenda tunawaeleza kuwa waongeze maeneo ya kulima. Lakini pamoja na hilo Kuna moja ambalo linahitaji tulizungumze zaidi ambalo hata mheshimiwa Rais amelizungumza akiwa Morogoro alisema tuongeze tija sehemu tunapolima ili tupate mazao zaidi,” amesema.

Profesa Mkenda akitolea mfano wa kuongeza tija ya mazao alisema: “Ukiangalia takwimu Kahawa yetu ya Arabika msimu wa 2020/21 tumepata Dola milioni 82 tumepata kwasababu tija yetu ipo chini ambako kwa mti mmoja ni gram 300 hadi 350 tukienda kwenye kilogram 1 hadi kilogram 1.5 kwa maeneo haya haya tunayolima tungeongeza kipatochetu cha fedha za kigeni kutoka Dola milioni 82 na kuongeza kiasi cha Sh milioni 47.

Aliongez: “Si suala la kusema kuongeza sehemu ya kulima bali muhimu ni kuongeza uzalishaji sehemu tunayolima,” amesema.

Akizungumzia kuhusu Kahawa aina ya Robusta alisema Kahawa hiyo yote ikiuzwa hadi nje tunapata dola milioni 52, kwa mti mmoja tunapata gramu 500 hadi 700 lakini tija bora kwa mti mmoja tunapata kilogram 1 hadi kilogram 2.

“Kama tungeenda kwenye tija nzuri mti mmoja tungetoka kwenye Dola mil. 52 na kupata Dola mil. 157 hivyo kama alivyosema Rais Samia Suluhu Hassan tutakwenda nalo kama tulivyoliombea katika bajeti,” alisema Waziri Mkenda.

Alisema kuwa ili kufanikisha hilo watashikamana na Bodi ya Kahawa kama ambavyo wamekuwa wakifanya Katika bodi nyingine za Korosho, Pamba na nyingine ili kuongeza tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles