27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAKILI KESI YA BILIONEA MSUYA AUGUA GHAFLA

Na Upendo Mosha-MOSHI

KESI ya mauaji ya mfanyabiahara wa madini, Bilionea  Erasto Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasa 22, iliyokuwa inaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, jana iliahirishwa    baada wakili wa utetezi, John Lundu kuugua ghafla.

Kesi hiyo iliahirishwa baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula, kumwomba Jaji anayesikiliza shauri hilo, Salma Maghimbi, kuiahirisha kutokana Wakili anayemtetea mshitakiwa wanne, sita, na saba  John Lundu kuugua.

Kwa sababu hiyo Lundu alishindwa kumuhoji shahidi wa kwanza katika kesi  hiyo ambaye ni Mtaalamu wa Makosa ya Mtandao Detective CPL, G. 630 Selaman Mwaipopo.

“Wakili anayemtetea mshitakiwa wa wa nne, sita na saba, John Lundu, alikuwa amebaki kumuhoji shahidi wetu wa kwanza katika kesi ndani ya kesi na leo (jana) ameshindwa kufika mahakamani kutokana na kuugua.

“Hivyo kutokana na sababu hiyo, tunaiomba mahakama iahirishe shauri hili mpaka kesho (leo),” alisema Chavula

Alisema katika kesi ndani ya kesi upande wa Jamhuri ulikuwa umeandaa mashahidi wawili ambao ni Detective CPL, G. 630 Selaman Mwaipopo na  Detective Koplo Jawadu Mhenga.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Wakili wa Utetezi, Emanuel Safari aliyesema kuwa ni vema mahakama ikazingatia ombi hilo kutokana na umuhimu mkubwa washahidi huyo kuhojiwa  na wakili wa utetezi, John Lundu.

Jaji Salma Maghimbi aliwataka mashahidi wote wawili wa upande wa mashtaka kufika mahakamani leo ili kesi ndani ya kesi iendelea na akaagiza washtakiwa wote warudishwe rumande.

Mbali na wakili John Lundu kushindwa kufika mahakamani kutokana na kuugua, pia mawakili wawili wa upande wa utetezi, Godson Ndusyepo anayemtetea mshitakiwa wa kwanza na Majura Magafu anayemtetea mshitakiwa wa pili na watatu hawakuwapo mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles