27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WAKILI AKIRI TRUMP ALIMLIPA MCHEZA FILAMU ZA NGONO

WASHINGTON, MAREKANI


MWANASHERIA mpya katika kundi la mawakili wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Rudy Giuliani amesema bosi wake huyo alimrudishia mwanasheria wake mwingine dola 130,000 alizomlipa mchezaji wa filamu za ngono Stormy Daniels.

Daniels anadai alikuwa na uhusiano na Rais Trump, ambaye amekuwa akina hilo vikali.

Stormy alikabidhiwa fedha hizo na mwanasheria Michael Cohen siku chache kabla ya uchaguzi wa rais, mwishoni mwa 2016 ambao Trump alishinda.

Hata hivyo, akizungumza na Kituo cha Televisheni cha Fox News cha hapa, Giuliani, ambaye ni meya wa zamani wa New York alisema malipo hayo hayakuwa na uhusiano wowote na kampeni za Trump, na kuwa hayakukiuka sheria yoyote.

Lakini wataalamu wengine wa masuala ya sheria hawakubaliani naye kwa hoja ya muda na mazingira yalimofanyika malipo hayo.

Wakosoaji wanaamini Trump aliyekuwa anaandamwa na kashfa nyingine ya kutoa matamshi machafu kuhusu wanawake, alikuwa akitaka kumnyamazisha Daniels asifichue uhusiano wao, hali ambayo ingeweza kumnyima ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles