27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi Magomeni Kota wamuangukia Rais Samia

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kupata haki zao za msingi ikiwemo kupewa funguo ili waendelee kuishi ndani ya nyumba hizo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, mmoja wa wakazi hao, Zamzam Mwalim amesema ni miaka 12 sasa anaishi katika maisha ya tabu kwa ajili ya kupisha ujenzi wa nyumba hizo.

“Mwaka 2011 tulivunjiwa nyumba na tukapewa mikataba wote watu 644 na mikataba hiyo tulipewa na Halmashauri ya Kinondoni kupitia amri ya mahakama iliyothibitisha kuwa sisi ni wakazi halali na wamiliki wa hizi nyumba,” amesema Zamzam.

Amesema baada ya nyumba kukamilika kujengwa katik zoezi la kukabidhiwa funguo watu 61 wameshindwa kupatiwa funguo hadi sasa.

Amesema wapo baadhi ya watu wanaoendelea kuishi katika nyumba hizo ambao hawana mkataba na hawakuwa wakaazi wa Magomeni Kota.

“Tunamuomba rais na viongozi wake kupitia upya suala la uhakiki ili kuweza kupata haki zetu za msingi tunaimani na Rais Samia na anaweza kutusaidia,”amesema Zamzam.

Upande wake Wakili wa wakazi hao wa Magomeni Kota, Twaha Taslima amesema ni vyema kwa wakala wa Majengo(TBA) kutumia busara ya maridhiano kwa kukaa pamoja ili kuweza kulipatia ufumbuzi suala hili.

Amesema kwa mujibu wa TBA inawataka wakazi hao kwenda mahakamani kitu ambacho kinaweza kuendelea kuleta mgongano.

“Kuishtaki taasisi yoyote ya Serikali ni lazima barua yako ipitie kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa mujibu wa sheria atatakiwa asitishe eneo kwa kipindi cha miezi mitatu lisifanye kazi,” amesema Taslima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles