26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WAKAZI JANGWANI WAPAMBANA NA POLISI KUZUIA BOMOA BOMOA

 

Wakazi wa Jangwani jijini Dar es Salaam, leo wamepambana na polisi na kusababisha vurugu katika barabara ya Morogoro.

Wananchi hao walikuwa wakizuia tingatinga la bomoa bomoa lisibomoe nyumba zao zilizoko bondeni kwa kuwarushia mawe hatua iliyowalazimu kutoa taarifa  polisi ambao walikuja baada ya muda mfupi na kuwatawanya kwa kufyatua risasi na mabomu ya machozi huku wananchi hao akiwarushia mawe polisi hao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wananchi hao wamedhibitiwa na zoezi la ubomoaji linaendelea.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles